Thursday, January 16

ZECO wajitetea kuingia Robo fainali ya mwisho katika mashindano ya mawizara Pemba.

NA ABDI SULEIMAN.

MABINGWA wa Tetezi wa Mashindano ya Mawizara Pemba, wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali katika mashindano hayo yanayoendelea Kisiwani Pemba, kwa kwachapa kwa mikwaju ya penant 5-2.

Mchezo huo wa Robo fainali ya mwisho katika mashindano hayo, ililazimika mshindi kupatikana kwa mikwaju ya Penant baada ya timu hizo kufungana bao 2-2.

Mtanange huo ulionekana kutawaliwa na ubabe kiwanjani hapo, baraza la mji wakionekana kuwa na kasi uwanjani hapo, ikachukua dakika ya sita tu baraza la mji kupata bao la kuongoza kupitia kwa Abdalla Said, huku ZECO ikasawazisha kupitia kwa Ramadhan Abdalla dakika ya 18.

Hata hivyo baraza la mji iliweza kuandika bao la pili dakika ya 54 kupitia kwa Khamis Haji hali iliyowafanya ZECO kutokukata tama na kusawazisha bao dakika ya 88 kupitia kwa Ramadhani Abdalla.

Kwa matokeo hayo timu zilizotinga hatua ya nusu fainali ni ZECO, Afya, Utalii na Mawasiliano.