Monday, November 25

Aina ya sita ya vyakula ambavyo vikichanganywa hugeuka sumu

Kila binadamu ana kile alichojaaliwa na Mungu. Siku zote anachoamua mmoja kula huenda kikawa sumu kwa mwingine.

Chakula anachokula mtu kinaenda sanjari na hali ya kiafya. Wengine huumwa hadi kusababisha kupoteza uhai na hii ni baada tu ya kupendelea kuchanganya chakula.

Mtu mmoja anaweza kula sawa na kwa urahisi, ila kwa mwingine kikageuka sumu.

Hali hii huchochewa zaidi na matokeo ya baadae pale unaposhindwa kuweka mchanganyiko sahihi na wenye afya zaidi .

Kila aina chakula ina faida zake, ila kinapochanganywa kinaweza kusababisha shida kwa mtu.

Kwa watu ambao wanataka kuchanganya lishe ili kupunguza unene na vichocheo vyake ni vyema kushauriana na wataalamu jinsi ya kupanga lishe bora.

Mtaalam wa lishe wa Nigeria Habiba Haruna ameiambia BBC kuhusu aina sita za chakula ambazo zinaweza kuwa sumu kwa mtu yeyote.

Samaki na Maziwa

samaki

Samaki na Maziwa ni vyakula vyenye virutubisho lukuki na kuvichanganya katika sehemu moja vinaweza visiwe na uwezo wa kutengeneza virutubisho sahihi na hii inaweza kuleta shida baadaye.

Mwili wa binadamu hauhitaji vyakula vya aina tofauti vyenye kemikali za aina moja kuchanganywa. Huweza kusababisha sumu itakayopelekea mtu kutapika na hata kuharisha.

Maji ya limao na Maziwa

Maziwa na limao huwa haviwezi kukaa sehemu moja kwani vikichanganywa lazima maziwa yaweze kukatika.

Ikiwa mtu atachanganya maziwa na maji ya limao anaweza kutengenezea sumu, vilevile yanaweza kuleta shida katika moyo.

Karanga na Mafuta ya mzeituni

ayaba da gyada

CHANZO CHA PICHA,OTHER

Karanga ina umuhimu mkubwa sana katika mwili wa binadamu na hutumika katika sehemu nyingi sana.

Pia karanga ina kiwango kikubwa sana cha protini na wanga, vilevile Karanga ni moja ya virutubisho muhimu katika lishe, haswa kwa wale ambao wanataka kupunguza uzito.

Kwa mafuta ya mzeituni yanamsaada mkubwa pia hasa katika masuala ya tiba kwa baadhi ya magonjwa, lakini mchanganyiko wa mafuta hayo na karanga yanaleta shida ila inashauriwa kutumika pale moja inapokosekana lakini sio kwa pamoja.

Dawa pamoja na sharubati ya limao

limao

Kuchukua dawa na kuchanganya na kitu chenye gesi ina madhara makubwa, wataalamu wanasema kuwa kunywa dawa na soda kama fanta au Coca-Cola inaweza kukusababishia kifo kutokana tu ongezeko kubwa la gesi.

Ameongeza kwa kusema kuwa limao au kinywanji chochote chenye gesi hakipaswi kuchanganywa na dawa ni hatari.

Nyama na mayai mabichi

mayai

Kuchanganya nyama ambayo haijaungwa na mayai mabichi inaweza kusababishia matatizo katika mwili wa binadamu.

Inaweza kuwa sumu kwa wengine, zingine zinaweza kusababisha kutapika na kuhara kwa sababu haifai kutumika hivyo.

Nyama mbichi inaweza kusababisha athari ikiwa usindikaji wake haufuatwi ili kupunguza kiwango cha virutubishi vilivyomo.

Mtaalamu anasema kuwa mayai mabichi hayana virutubisho kwenye mwili wa binadamu, yakiwa bado kwenye hali hiyo hayapaswi kuliwa mpaka pale yatakapochemshwa au kukaangwa ndio hujenga mwili.

“Mayai mabichi sio ya kuyaamini,” Anasema Mtaalamu wa chakula kutoka Nigeria, Habiba Haruna.

Wataalamu wanashauri watu kula kile wanajua kitakuwa na faida na haitawasababishia matatizo yoyote.

Kujaribu kitu kipya kunaweza kuwa na faida kwa wengine lakini pia kunaweza kuwa na madhara.

Kuna aina nyingi sana ya vyakula ambavyo vikichangwanywa vinaweza sababisha madhara.

Mtu anapaswa kuwa mwangalifu katika uchaguzi wa vyakula ni vyema aweke vyeme virutubisho na kuepuka kuvichanganya.

CHANZO CHA HABARI BBC