Wednesday, January 15

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi Amefungua Mafunzo ya Wajasiriamali na Kuipongeza Benki Ya CRDB Kwa Tamasha La Kihistoria La Kizimkazi.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwasalimia Wananchi wa Kijiji cha Kizimkazi wakati akiwasili katika Viwanja vya Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi kwa ajili ya Ufunguzi waMafunzo ya Wajasiriamali na Uzinduzi wa Tamasha la Kizimkazi, akiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya CRDB.Bi.TullyEsther Mwambapa, wakielekea katika ukumbi.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya CRDB, TullyEsther Mwambapa, alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi, kufungua Mafunzo ya Wajasiriamali wa Kizimkazi na kulifungua Tamasha la Kizimkazi, ufunguzi huo umefanyika katika ukumbi wa Mitihani wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano kwa ajili ya ufunguzi wa Mafunzo ya Wajasiriamali wa Kizimkazi na kufungua Tamasha la Kizimkazi  katika ukumbi wa mitihani wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi  Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwananchi wa Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja akisoma risala ya Wajasiriamali wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Wajasiriamali yaliofanyika katika ukumbi wa Mitihani wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi.Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mke wa Rais wa Zanzibar.Mama Mariam Mwinyi.

 

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya CRDB.Bi. TullyEsther Mwambapa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wajasiriamali wa Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja,  alisema Benki ya CRDB imedhamiria kubadirisha maisha ya wana Kizimkazi kupitia sera yake ya kurudisha kwenye jamii ambapo kila mwaka Benki hutenga asilimia moja ya faida yake kuwekeza katika jamii. Sambamba na ufadhili wa tamasha la Kizimkazi, Benki ya CRDB  imekamilisha ujenzi wa miradi miwili ya maendeleo ambayo itakabidhiwa kwa Mgeni Rasmi  wa Tamasha la Kizimkazi 2021 ambae ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan  siku ya kilele cha tamasha Agosti 28.
“Imani yetu ni kuwa fursa zitakazopatikana kupitia Tamasha la Kizimkazi zitaleta hamasa kubwa na kuchochea shughuli za kiuchumi hapa Kizimkazi na hivo kuongeza mchango wa wana Kizimkazi katika kutekeleza dhana ya Uchumi wa Bluu ambayo inaongoza Serikali ya Awamu ya 8 ya Mapinduzi ya Zanzibar” aliongeza Tully.
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa wananchi wa Kizimkazi pamoja na Uzinduzi wa Tamasha la Kizimkazi 2021,ufunguzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Skuli wa Sekondari ya Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja, kwa udhamini wa Benki ya CRDB.
“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuwawezesha wajasiriamali ambapo pamoja na mambo mengine Serikali imeanzisha mfuko wa uwezeshaji kwa wajasiriamali, imefanya uteuzi wa Katibu Mkuu maalum anaeshughulikia masuala ya uwezeshaji lakini pia imeendelea na juhudi za kuhamasisha taasisi za kifedha ikiwemo Benki ya CRDB kusaidia uwezeshaji kwa wajasiriamali” alisisititiza Mama. Mariam.
Pamoja na kupongeza shughuli za kitamaduni, sanaa na michezo zitakazofanyika katika tamasha hilo, Mh. Mariam Mwinyi ameiomba Benki ya CRDB kuendelea kusaidia wakazi wa Kizimkazi katika eneo la elimu hasa kwa kusaidia upatikanaji wa vifaa ya maabara mashuleni. Sambamba na wito huo kwa Benki ya CRDB, Mh. Mariam alitoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanasimamia vyema malezi ya watoto na kuwahimiza katika elimu ambayo itawasadia  katika maisha yao huku akitoa mfano wa Rais wa Jamuhuri ya Muugano wa Tanzania,       Mhe. Samia Suluhu Hassan ambae ni mzaliwa wa Kizimkazi.
Wananchi wa Kijiji cha Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Mgeni Rasmi Mke wa Rais wa Zanzibar. Mama Mariam Mwinyi, akizungumza na kuwahutubia wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mafunzo ya Wajasiriamali pamoja na Ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi uliofanyika katika ukumbi wa mitihani wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.
Wananchi wa Kijiji cha Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Mgeni Rasmi Mke wa Rais wa Zanzibar. Mama Mariam Mwinyi, akizungumza na kuwahutubia wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mafunzo ya Wajasiriamali pamoja na Ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi uliofanyika katika ukumbi wa mitihani wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.
Wananchi wa Kijiji cha Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Mgeni Rasmi Mke wa Rais wa Zanzibar. Mama Mariam Mwinyi, akizungumza na kuwahutubia wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mafunzo ya Wajasiriamali pamoja na Ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi uliofanyika katika ukumbi wa mitihani wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Wazee wa Kizimkazi baada ya Ufunguzi wa Mafunzo ya Wajasiriamali pamoja Ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi na (kushoto kwake) Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya CRDB.Bi. TullyEsther Mwambapa na Mkuu wa Wilaya ya Kati Bw. Rashid Makame Shamsi na (kulia kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Rashid Hadadi Rashid na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Bi. Marina Joel  Thomas.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi  akizungumza na kubadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya CRDB.Bi. TullyEsther Mwambapa, baada ya kumalizika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya Wajasiriamali na Ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi  uliofanyika katika ukumbi wa mitihani Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi  akiagana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya CRDB.Bi. TullyEsther Mwambapa, baada ya kumalizika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya Wajasiriamali na Ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi  uliofanyika katika ukumbi wa mitihani Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.