Thursday, January 16

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 27.08.2021: Ronaldo, Mbappe, Kane, Kounde, Traore, Aubameyang

Cristiano Ronaldo alijiunga na Juventuskwa mkataba wa thamani ya euro milioni 112 (£99.2m) mwaka 2018

Manchester City na Juventus zimekubaliana kuhusu uhamisho wa mshambuliaji mreno Cristiano Ronaldo, 36, kujiunga na klabu hiyo ya City. (AS – in Spanish)

Juventus wanataka kati ya £21m-25m kwa ajili ya Ronaldo, huku City ikitarajiwa kumpa mkataba wa miaka 2. (Guardian)

Klabu hiyo ya Italia inatarajia Ronaldo atabakia klabuni hapo lakini wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa City mbrazil Gabriel Jesus, 24, kama mbadala wake. (Sky Sports)

 

Wolverhampton Wanderers imekataa ofa ya mkopo kwa ajili ya winga wake raia wa Hispania Adama Traore, 25, kutoka Tottenham Hotspur, wakitaka kumbakiza. (Telegraph)

Adama Traore

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Winga wa Wolverhampton Wanderers Adama Traore

West Ham United inamnyemelea mshambuliaji wa CSKA Moscow na Croatia Nikola Vlasic, 23, wakiendelea kutafuta mbadala wa kiungo mshambuliaji wa Manchester United na England Jesse Lingard. (Sky Sports)

Watford imeanza mazungumzo na Tottenham kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo mfaransa Moussa Sissoko, 32. (Fabrizio Romano)

Paris St-Germain inaendelea kusaka wachezaji akiwemo kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 28, na mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21, wakati huu wakijiandaa kumkosa Kylian Mbappe. (L’Equipe, via Mail)

Manchester United midfielder Paul Pogba

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba

Real Madrid imeongeza dau lake kufikia £145m kwa ajili ya mshambuliaji wa Ufaransa na PSG Mbappe, 22, baada ya dau lake la awali la £137m kukataliwa. (Sky Sports)

Manchester United imemkosa winga wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 Noni Madueke, 19, baada ya nyota huyo kusaini mkataba mpya na klabu yake ya PSV Eindhoven. (Mirror)

Nahodha wa Tottenham na England Harry Kane yuko kwenye mazungumzo kuhusu kuboresha mkataba wake. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, anatarajia mshahara utakaofikia £400,000 kwa wiki kupitia maboresho hayo ya mkataba baada ya kuamua kusalia klabuni hapo msimu huu. (Times – subscription required)

Harry Kane

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Harry Kane yuko kwenye mazungumzo kuhusu kuboresha mkataba wake

Chelsea wanakaribia kabisa kumsajili mlinzi wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, 22, katika uhamisho utakaogharimu £42m. (Sky Italia, via Star)

Wakati huo huo mlinzi wa kati wa Chelsea Kurt Zouma, 26, atafanyiwa vipimo vya afya kabla ya mfaransa huyo kusaini mkataba wa miaka 5 West ham kwa uhamisho utakaogharimu £26m. (Sun)

Tottenham imeanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Juventus na Marekani Weston McKennie, 22 uhamisho utakaogharimu £40mil(Independent)

Pierre-Emerick Aubameyang

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Mikel Arteta ametupilia mbali uwezekano wa mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang kuondoka

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta ametupilia mbali uwezekano wa nahodha na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang kuondoka klabuni hapo. (ESPN)

Everton inamtaka mshambuliaji wa Brighton mfaransa Neal Maupay, 25. (Sky Sports)

Manchester United inataka kusajili kiungo kabla ya dirisha la usajili kufungwa, lakini itawapasa kusubiri kuona kama wanaweza kumpata kiungo wa England na West Ham Declan Rice, 22. (Independent)

CHANZO CHA HABARI BBC