Thursday, January 16

Vita vya Afghanistan: Bonde ‘lililoshindikana’ lililoko umbali wa saa moja kutoka Kabul

Taliban wamedhibiti maeneo karibu yote nchi nzima kasoro eneo hili tu la jimbo la Panjshir.

Sio mara ya kwanza kwa bonde hilo la kushangaza la Panjshir kuwa kielelezo cha misukosuko ya kihistoria nchini Afghanistan – ilikuwa ngome muhimu wakati wa vita dhidi ya vikosi vya jeshi la Wasoviet katika miaka ya 1980, na Taliban katika miaka ya ’90.

Kundi lililoweka ngome yake kwenye bonde hilo sasa ni- National Resistance Front of Afghanistan (NRF) – linalokumbusha dunia kuhusu nafasi na nguvu ya bonde hilo.

“Jeshi la serikali na washirika wake walishindwa …na Taliban kwa miaka 25 iliyopita walijaribu kulichukua lakini walishindwa… , walikutana na kipigo kibaya,” Ali Nazary, kiongozi wa NRF wa masuala ya mahusiano ya kimataifa ameiambia BBC.

Bonde hilo refu, lenye kina kirefu na lenye kutawaliwa na vumbi la udongo liko maili 75 kama kilometa 120km – kusini magharibi kwenda kaskazini mashariki – huko kaskazini mwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul. Bonde hilo linazungukwa na milima mirefu yenye urefu wa mpaka futi 9,800 kama kilometa 3 kutoka usawa wa bonde lenyewe.

Milima hii inatumika kama vikwazo vinavyowasaidia watu wanaoishi apo wasiweze kufikiwa kirahisi, inawalinda.

Kuna barabara nyembamba ya kuingia kwenye eneo la bonde hilo ambayo hupita katikati ya miamba mikubwa ya mawe na mto Panjshir.

“Hili sio bonde moja. Ukishaingia ndani utakuwa kuna vibonde vidogovidogo karibu 21 ilivyounganika,” anasema Shakib Sharifi, aliyewahi kuishi hapo wakati wa utoto wake, lakini aliondoka Afghanistan baada ya Taliban kushika hatamu.

“Kihistoria bonde hili la Panjshir linafahamika pia kwa uchimbaji wa madini,” anasema Elisabeth Leake, profesa kutoka chuo kikuu cha Leeds, Uingereza.Maelfu ya wanapiganaji wanaolipinga kundi la Taliban nchini Afghanistan wanaripotiwa kukabiliana na kundi hilo wakiwa wamejificha kwenye bonde lililo ndani ndani, lenye njia jembamba la kuingilia – takriban maili 30 kutoka mji mkuu, Kabul.

Bonde hili lina mabwawa yanayofua umeme. Marekani ilisaidia ujenzi wa barabara za eneo hilo na kuweka mkongo wa radio ambao unapokea mawasiliano kutoka Kabul. Kambi ya wanajeshi wa anga wa Marekani, ambayo awali ilijengwa na wasovieti katika miaka ya 1950 – pia iko karibu tu na mdomo wa bonde hilo.

‘Watu wenye akili’

Kati ya watu 150,000 na 200,000 wanaishi katika bonde hilo. Wengi wakizungumza Dari – moja ya lugha kuu nchini Afghanistan – na wanatokea kwenye jamii ya kabila la Tajik.

Kabila hilo ni kama robo ya watu wote milioni 38 wa nchi hiyo – lakini watu wanaoishi hapa (Panjshiris) wana utambulisho wao.

Bwana Sharifi – ambaye mpaka hivi karibuni alikuwa mkurugenzi mkuu wa mipango kwenye wizara ya kilimo ya Afghanistan – anawaelezea watu wa eneo hilo kama wenye akili sana, “pengine ndiyo watu wenye akili kushinda wote Afghanistan”.

Panjshir Valley, Afghanistan, 2019

CHANZO CHA PICHA,ALAMY

Anasema watu hao hawapatani na Taliban na wanasifa ya ugomvi – lakini ugomvi wao ni wa namna nzuri”. Ushindi wa kihistoria dhidi ya Waingereza, wasovieti na Taliban ulizidi kuwatia moyo zaidi watu “.

Baada ya Taliban kushindwa na kuondolewa madarakani mwaka 2001, bonde hilo likapandishwa hadhi kutoka wilaya na kuwa jimbo. Moja ya majimbo madogo nchini Afghanistan.

“Uamuzi wa kuipandisha hadhi na kuwa jimbo ulikuwa uamuzi wa utata,” anasema Dkt. Antonio Giustozzi, mtafiti mwandamizi kutoka Royal United Services Institute (RUSI)

“Wapiganaji wa Panjshiri walikuwa na nguvu sana katika miaka ya 2000s’, alifafanua. Walisaidia kuirejesha Kabul na kuwa “mshirika namba moja”.

Panjshir Valley, Afghanistan, 2011

CHANZO CHA PICHA,ALAMY

Viongozi wa Panjshiri wakapewa nafasi maarufu kwenye serikali na jeshi.

Bonde hilo likawa huru na likawa bonde pekee nchini Afghanistan lililoogozwa na magavana wenye asili ya hapo, na sio kutoka nje ya eneo hilo.

“Kawaida gavana anatakiwa kuwa mtiifu kwa serikali kuliko watu anaowaongoza, kwa Punshir, ilikuwa tofauti,” anasema Dkt. Giustozzi.

Bonde lilikoa kimkakati

Kwa mujibu wa Dk. Giustozzi, kuna uwezekano kuwa yapo mabonde mengi yanayofanana na hilo nchini Afghanistan. Lakini ukaribu na barabara kuu kaskazini mwa Kabul unaipa bonde hilo “umuhimu mkubwa wa kimkakati”.

Afghan resistance movement and anti-Taliban uprising forces personnel. Panjshir province, Afghanistan, August 2021

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Wapiganaji wapinzani wa Taliban katika jimbo la Panjshir

Bwana Sharifi anasema umuhimu wa bonde hili la Panjshir ni muunganiko wa sababu nyingi.

“Sio kwa sababu ya uwepo wa maeneo mengi ya kujificha kwenye bonde hilo wakati wa mapambano, sio kwa sababu ya jiografia yake ya milima, sio kwa sababu ya kiburi cha kujivunia walichonacho Panjshir . Ni mambo yote hayo kwa pamoja. Sababu moja moja inaweza kuonekana sehemu nyingi nchini Afghanistan.”

“Maafisa wa serikali ya Afghan wenye mahusiano na Panjshir walipeleka silaha nyingi kwenye bonde hilo kwa sababu walikuwa na hofu kuhusu marais Karzai na Ghani, lakini miwshowe ni Taliban ndio waliokuwa na hofu zaidi.”

A portrait of Ahmad Massoud, Panjshir Valley, Afghanistan, September 5, 2019

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Ahmad Massoud 2019

Mtu anayeongoza wapiganaji wa Panjshir wanaopingana na Taliban ni kijana wa miaka 32 anaitwa Ahmad Massoud – mtoto wa aliyekuwa kiongozi hapo kati ya miaka ya 1980s na ’90s, Ahmad Shah Massoud.

Baba yake aliyejulikana kwa jina la utani kama “Simba wa Panjshir”, alikuwa kamanda wa Mujahidina aliyeongoza kuwafurushwa Wasoviet na Taliban waliotaka kuvamia bonde hilo.

Massoud aliwahi kusema kwamba wapiganaji wake wanapata msaada wa kijeshi kutoka kwa baadhi ya maafisa wa jeshi la Afghanistan na jeshi maalumu la taifa hilo.

Ni bonde lililoshindikana

Kati ya mwaka 1980 na 1985, wasovieti walianzisha mashambulizi ya ardhi na anga. Wapiganaji wa Urusi waliokuwa na uzoefu mdogo na eneo hilo, walishambuliwa vibaya.

Wasovieti walijeruhiwa maelfu kwa maelfu kutoka kila upande- anasema Sharifi.

Portraits of Ahmad Shah Massoud, Panjshir Valley, Afghanistan, 2009

CHANZO CHA PICHA,ALAMY

Dkt Giustozzi anasema vikosi vya Soviets vilifanikiwa kuliteka bonde hilo lakini kwa muda mfupi.

“Warusi hawakuona maana ya kukaa pale na kuwaweka wanajeshi wake pale ilikuwa changamoto kubwa,” anasema. “Walitaka kulinda barabara kuu ya kaskazini kusini, lakini mapigano yalizuka katika maeneo mengine ya karibu.”

Rusting helicopter from Soviet invasion of Afghanistan in 1979, Panjshir Valley, Afghanistan, 2015

CHANZO CHA PICHA,ALAMY

Maelezo ya picha,Picha ya mwaka 2015 ikionyeha helkopta ya Urusi, iliyotumika wakati uvamizi wa Soviet nchini Afghanistan mwaka 1979

Silaha, vifaru na ndege ziliachwa zikiota kutu kwenye bonde hili la Panjshir Valley – kama urithi wa kampeni za kijeshi za Soviet zilizoshindwa.

Dk. Giustozzi anasema katika kipindi hicho Massoud alikuwa tofauti na viongozi wengine wa waasi. “Alikuwa msomi, anayeweza kuzungumza kifaransa, anaongeta taratibu na alikuwa mcheshi.

Hata hivyo Massoud aliuawa mwaka 2001 na kundi la al-Qaeda, siku mbili kabla ya mashambulzi ya septemba 11, 2001 yaliyofanywa na kundi hilo. Massoud akatangazwa shujaa wa taifa na aliyekuwa rais wa Afghanistan Hamid Karzai.

Nini kinafuata?

Ahmad Massoud, arrives to attend and address a gathering at the tomb of his late father, Panjshir province, Afghanistan, July 5, 2021

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Ahmad Massoud alipotembelea maeneo ya kaburi alikozikwa baba yake, Julai 2021.

Ahmad Massoud aliyekuwa na miaka 12 wakati baba yake anafariki ni msomi aliyesoma London Uingereza.

“Ana haiba ya baba yake, lakini hajapata majaribu ya kuongoza vita,” anasema Dk. Giustozzi. “Pia anahitaji ujuzi wa kufanya mazungumza na kujadiliana kuhusu mgawanyo wa madaraka kitaifa. Kwa sababu ni mgeni na hana cha kupoteza.”

Prof Leake anasema “Anafahamu wazi kuhusu alichorithi na umuhimu wa historia ya baba yake – anaweza kuendeleza urithi huu hizi kwa ushiriki wake kimataifa.

“Lakini kwa sasa mambo ni tofauti. Talibani wamechukua udhibiti wa karibu majiji yote makubwa na miji iliyo karibu na bonde hilo – hivyo uingzwa wa bidhaa na silaha umekuwa mkubwa. Hili linaleta utofauti.”

Massoud mwenye ameshaomba msaada. “Kama wababe wa vita wa Taliban wataanzisha mashambulizi, bila shaka watakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwetu… Ingawa tunafahamu kuwa vikosi vyetu na silaha havijitoshelezi,” aliandika kwenye gazeti la Washington.

“Zitapungua haraka, isipokuwa kama marafiki zetu kutoka Magharibu watatafuta namna ya kutusaidia bila kuchelewa.”

CHANZO CHA HABARI BBC