Monday, November 25

Je, uvumbuzi wa kubadili fikra za ubongo kwa kutumia vilevi ulianza lini?

Binadamu mara zote huwa wanabadilisha dunia : Binadamu anabadilisha msitu kuwa shamba kwa kupanda mimea na kufuga wanyama.

Binadamu huwa hawabadili mazingira yao ya nje tu ila wanabadili hata jinsi ya kufikiri, kuongea kwa kuzingatia imani zao, simulizi, falsafa na saikolojia .

Suala lingine ni kubadili akili zao pia katika ubongo , na wanafanya hivyo kwa kutumia kemikali.

Wengi hutumia mimea kutengeneza .

Ingawa wengine wanapenda kahawa na chai.

Dawa za kulevya na pombe uleta mihemko na kubadili uhalisia.

Binadamu wanabadilisha ubongo kwa namna mbalimbali za kijamii, kitabibu na kiimani.

Wakati mwingine wanyama pori hula matunda yaliyo na chachu ya mihemko, lakini kuna ushahidi mdogo kuwa huwabadili kiakili.

Hivyo binadamu ni wanyama wa ajabu ambao hunywa pombe na kulewa.

 

Lakini ni lini, wapi na kwanini watu walianza kutumia vilevi?

pombe

Ukiangalia namna ambavyo pombe na dawa zinavyopendwa unaweza kudhani kuwa kulewa ni jambo la kale ambalo lilikuepo enzi na enzi na kuwa utamaduni katika historia.

Baadhi ya watafiti wanasema katika michoro ya mapango kuna michoro inayoonesha binadamu ambao walikuwa na hali za kubadilisha ufahamu.

Wengine labda walivutiwa na ushahidi wa kufikirika zaidi ya ushahidi wenye uhalisia , unaoonesha jinsi dawa za kulevya zinavyobadili fahamu za binadamu.

Hata hivyo kuna ushahidi mdogo wa akiolojia wa utumiaji wa dawa, kihistoria ya Jamii ya wawindaji wa Afrika, ambao labda waliishi maisha sawa na watu wa kale.

w
Maelezo ya picha,Jamii ya Wahadzabe

Ushahidi unaonesha kuhusu binadamu wa kale kuhusu dawa ni kutoka kwa mmea unaoitwa kaishe, ulitumiwa na watu wa kale kama tiba na ulikuwa unawafanya watu wawe kama wamechanganyikiwa kwa muda.

Lakini suala la watu wa kale kuwa na historia ya kutumia dawa bado halina jibu na kuna ushahidi mdogo sana kuwa wawindaji walitumia dawa.

Na labda walikwa wana namna yao ya maisha ambayo yalikuwa yanawahitaji kuyasahau kwa muda.

Kufanya mazoezi, kuota jua, mazingira, kukaa na marafiki na familia ni husaidia .

Dawa huwa hatari pia; ni sawa na wanavyosema usiendeshe gari ukiwa umekunywa pombe ni hatari, hivyo ni hatari kwenda kuwinda ukiwa umelewa , ukikutana na simba porini ni vigumu kujiokoa.

Nje ya Afrika

s

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Wakati wawindaji walipovuka Daraja la Beringia miaka 30,000 iliyopita kwenda Alaska na kuelekea kusini, walipata ushahidi mdogo wa matumizi ya kemikali.

Huko wawindaji walikuwa wamegundua tumbaku,coca na uyoga.

Lakini kwa sababu zozote zile Wamarekani wa kale walikuwa wamevutiwa kubadilika kwa mitazamo au fikra.

Lilikuwa tamasha la Columbia, watu wenye asili ya Marekani walikuwa wakitumia tumbaku na uyoga.

Walikuwa wa kwanza kuanza kutumia dawa za kulevya na baadaye ulaya iliiga.

Utamaduni huu ni wa zamani kwa Watu wa asili ya Marekani.

Miaka 1,000 iliyopata huko Bolivia kulikuwa na dawa za kulevya aina ya kokeni, hii ilikuwa safari ya kushangaza.

v

CHANZO CHA PICHA,BBC SPORT

Uvumbuzi wa pombe

Hatua kubwa katika mabadiliko haya ilikuwa uvumbuzi wa kilimo, kwa sababu kilifanya pombe iwezekane kutengenezwa.

Ilitengeneza sukari ya zaidi na wanga ambao, wakati zinapochanganywa inatengeneza uchachu wa kushangaza na wenye uwezo mkubwa kubadili mtu .

Binadamu walianzisha pombe tangu 7,000 BC. C., huko China.

Mvinyo ulianza kutengenezwa 6000 BC. C .Walitengeneza bia 3000 BC. C.

Marekani ,ndio wanahusishwa katika utengenezaji vilevi vya leo kama tequila, shisha na bia zinazotengenezwa na mahindi.

pombe

Wakati dawa ilionekana muhimu Marekani, Ulaya, Asia na Afrika walipendelea pombe.

Mvinyo ulipendelewa utamaduni wa Ugiriki na Roma ,na inahusishwa na utamaduni wa wayahudi na ukristo.

Ustaarabu na ulevi

Watafiti wanasema pombe na dawa za kulevya tangu enzi za milenia zilianzia kwa jamii ya wakulima wa awali.

Lakini kuna ushahidi mdogo kuwa wawindaji wa kale walikuwa wanatumia dawa au pombe hizo.

Hii inadhihirisha kuwa jamii ya wakulima ndio ilianzisha matumizi ya vilevi.Lakini kwanini?

Inawezekana kuwa ustaarabu huo waliopata ulisukuma kutokea kwa uzinduzi wa kila kitu kama nguo, vyungu,vyuma na dawa.

Labda pombe na dawa zilihamasisha ustaarabu pia : Kunywa pombe kunaweza kusaidia watu waweze kuwasiliana, kushirikiana, kuwa wabunifu, na kuwa na muhemko au nia ya kufanya kitu.

Na inawezekana kuwa salama kulewa mjini.

Uwezekano mbaya ni kwamba matumizi ya dawa kila mara yanaweza kumfanya mtu kushindwa kukabiliana na magonjwa.

Jamii kubwa huwa zinatengeneza matatizo makubwa kama vita, kukosa usawa katika utawala na utajiri .

Labda pale ambapo watu wanashindwa kubadili hali zao wanaamua kubadili mitazamo yao.

Ni tatizo kubwa. Kufikiria tu kuhusu jambo hilo kunanifanya nitake kunywa bia!

CHANZO CHA HABARI BBC