Mara nyingi malalamiko ya unyanyasaji unaofanyika majumbani hutolewa na wanawake. Theluthi moja ya wanawake hupitia unyanyasaji wa kimwili na kingono katika kipindi cha maisha yao, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.
Unyanyasaji ambao ni nadra sana kutokea na kujadiliwa ni unyanyasaji wa kingono dhidi ya mwanaume au unyanyasaji wa mwanaume ambaye amefanyiwa unyanyasaji na mtu wa familia yake.
Unyanyasaji wa nyumbani dhidi ya wanaume unachukuliwa kama kitu cha aibu katika jamii na mwanaume huteseka peke yake bila msaada wowote.
Kijana mmoja kutoka nchini Ukraine ambaye hakupenda kutaja jina lake aliielezea BBC unyanyasaji alioupitia.
Tunawasilisha taarifa yake hapa ambayo inajumuisha ushauri wa wataalamu wanaoelezea jinsi ya kutambua unyanyasaji wa kingono dhidi ya mwanaume na namna ya kukabiliana na unyanyasaji w nyumbani.
Mara ya kwanza ilivyotokea kwangu
Sijui kama marafiki zangu walikuwa hawaniamini. Ungenitazama kwa sura tu ungefikiri kwamba kila kitu kilikuwa sawa kwangu , Nilikuwa na uso wa tabasamu, marafiki, na pesa za kutosha, furaha na ungeliniona ni mtu anayejiamini. Sikuwa na sababu ya kuhofia tulipokuwa tukienda kutembea.
Hakunisumbua mbele ya watu wengine. Alikuwa tu anakuwa mwangalifu anapokuwa na mimi peke yetu.
Ilinijia akilini kwamba mke wangu amekuwa akinibaka kwa miaka 10.
Bi Ira alikuwa mwanamke wa kwanza katika maisha yangu. Yeye ndiye aliyeniomba nikutane naye.
Wazazi wangu waliniambia kwamba unapaswa kutafuta nyumba yako baada ya kuanza urafiki na msichana. Ilimaanisha kwamba kama nitampenda mtu fulani, ni lazima niondoke katika familia yetu na kupoteza makazi ya familia. Ni lazima nipoteze kila kitu katika siku moja na kuanza maisha yangu.
Kwangu mimi lilikuwa ni jambo lililonitia wasiwasi. Kwa hiyo niliingia katika mapenzi baada ya kujiwekea akiba kwa kadri nilivyoweza ili kuniwezesha kutengana na familia yetu.
Kukosa kujiamini
Mama yangu aliaibishwa na muonekano wangu. Sikuwa mtu wa kujiamini hata kidogo.
Uzoefu wangu wa kwanza wa ngono niliupata pamoja na Ira na wakati ule nilikuwa nimemtamani sana. Hiyo haikuwa imetosha. Lakini haikuwa hivyo. Kulikuwa na maumivu mengi na mfadhaiko. Mara ya kwanza nilipokutana naye kimwili ilituchukua kama muda wa tano hivi na baada ya hapo nikaanza kusikia maumivu mwili mzima.
Alikuwa na hisia kwamba kwa mwanaume tendo hilo kukamilika lazima mbegu za kiume zitoke na kwa wastani ilikuwa inachukua saa moja au saa mbili kufanikiwa na wakati mwingine ilibidi anichue.
Ngono inapaswa kuwa raha, lakini sikuwahi kupata raha kwa tendo hilo. Kwahiyo nilikuwa ninasema tu nikifanya kile alichokisema yeye.
Lakini baadaye nilikataa. Lakini Ira hakukoma. Yote hayo yaligeuka kuwa ubakaji.
Kuanza kukwama
Nililazimika kwenda ng’ambo kwa safari ndefu ya kikazi. Nilikuwa na wasiwasi wa kumkosa Bi Ira kwahiyo nikamuomba aje twende naye. Hata nilikuwa tayari kumuoa kabla ya kwenda ng’ambo. Lakini alikataa nisimuoe, lakini akaambatana nami katika safari ya ng’ambo.
Hapo ndipo matatizo yalipoanza. Nilikuwa na kazi nyingi za kufanya na nilitakiwa ku[pumzika, lakini wakati wote alikuwa akidai ngono.
Wakati mmoja, nilisema ndio, wakati mwingine nikasema ndio… alisema, “Ninataka ngono, ninataka zaidi. Nimekuwa nikiisubiri kwa muda .”
Nilikuwa ninamwambia, “Hapana, sitaki kufanya. Nataka kupumzika. Nimechoka.”
Baada ya hapo alikuwa kinipiga na sikuweza kufanya chochote . Alikuwa akinigwara kwa kucha zake mwilini na wakati mwingine natokwa damu. Alikuwa akinipiga makonde, lakini hakuwahi kunipiga usoni . Alikuwa akinipiga sehemu za mwili zinaofichwa na nguo-kwenye kifua, mgongoni na mikononi.
Sikuweza kumpiga kwasabababu nilifikiria kumpiga mwanamke ni shambulio na sio sahihi. Hivyo ndivyo wazazi wangu walivyonifundisha.
Nilikuwa dhaifu na nilijihisi mchovu, lakini sikuweza kukwepa.
Wakati mmoja hata nilijaribu kutafuta chumba ili nijitenge, nilale kwenye chumba change peke yangu ndani ya hoteli. Lakini sikujua lugha iliyokuwa ikizungumzwa. Hapo ndipo nilipohisi nimechanganyikiwa.
Niliogopa kurudi hotelini baada ya kazi. Ilikuwa inanibidi nizurure madukani kupoteza muda hadi maduka yafungwe. Nilikuwa nazurura kwenye baridi hata sikuwa na nguo za kujifunika na hali ya hewa ilikuwa ya baridi sana na ya unyevunyevu.
Hali hii ilinisababishia maambukizi ya njia ya mkojo na homa. Hata katika hali hii Ira hakunipa nafasi alinitaka kingono na nililazimika kufanya alichokifanya.
Jumamosi na Jumapili zilikuwa ni siku mbaya sana kwangu. Tulianza asubuhi hadi Jumapili jioni . Nilikuwa tu nahesabu ni siku ngapi zimebaki nirejee Ukraine. Nilifikiria uhusiano wetu ungelimalizika baada ya kwenda Ukraine-lakini hilo halikutokea.
‘Nilijaribu kutoroka, lakini sikufanikiwa ‘
Nilienda kuishi na wazazi wangu tena na hata nikaacha kukutana tena na Iran. Hatahivyo itanichukua miaka kupona.
Tulikuwa tunazozana kwenye simu mpaka wakati mwingine nalazimika kuizima na kumzuia asiweze kunipigaa.
Hata ningejaribu kujificha mahali fulani ndani ya nyumba alikuwa akinifuata na kukaa upande mwingine wa mlango. Alikuwa akinipigia simu na kuniambia kuwa mambo yatakuwa mazuri kuanzia sasa.
Hii ilinifanya niendelee kumuona kila mara. Nilikuwa naogopa sana kuishi peke yangu.
Mwanzoni nilijaribu sana kumuacha Iran. Alijaribu baadaye kidogo lakini baadaye akachoka . “Tunapaswa kuoana sasa,” alisema Ira. Mimi sikutaka kabisa kuaona naye, lakini tukaoana.
Iran alimuonea wivu kila mtu: marafiki zangu, familia yangu. Kokote kule nilikoenda ilibidi nimjulishe na nimpigie simu kila wakati. Alinitaka kila niendpo nimpigie simu “Kwani ni lazima uhudhurie mikutano?” “Kwanini nikutane na marafiki?” Ilibidi niwe nae wakati wote.
Hakutaka niende nae kokote kule – Wakati wote nilitumiwa kama kifaa cha kumfurahisha Ira.
Ira hakuwa na kazi – Nililipia nyumba yetu ya kuishi, nilipika na kufanya kazi za usafi wa nyuma.
Tulikodisha nyumba kubwa yenye bafu mbili. Ilikuwa ni marufuku kutumia bafu kubwa maana alinikataza. Alinilazimisha kusubiri kwanza yeye aoge baada ya saa nne za asubuhi, maana alisema nisimsumbue kwa kumuamsha nitakatiza usingizi wake na hakutaka kusumbuliwa.
Baadaye aliamua kuwa tutakuwa tunalala vyumba tofauti, lakini akaniambia mimi nisiwe ninafunga chumba changu , kwani sipaswi kuwa peke yangu.
Na mara kwa mara alipohisi nimefanya kosa lolote alinifokea kwa sauti kali naya juu akisema kuwa ataniua . Hii ilikuwa inatokea wara mara moja kwa siku.
Baada ya kunifokea alinilaumu sana kwa kumpandishia hasira yake, huku akiniambia vile angependa mumewe awe na jinsi angetaka afanye na kile cha kufanya.
Nilijihisi sina la kufanya na nilikuwa tayari kufanya lolote lile kusitisha hasira yake.
Nakumbuka wakati mmoja nilikwenda kwenye chumba cha chini cha nyumba yetu na kukaa ndani ya gari na kuanza kulia.
Ira alipita akaniona nikilia. Nilipoingia nyumbani alisema kuwa alikuwa amesikitika sana, lakini hakuweza kujizuwia kunilazimisha kulala naye.
Lakini siku iliyofuatia, unyanyasaji wa aina hiyo ulianza tena. Haikujalisha ni nini nilichofanya na ni kwa jinsi gani nilikuwa ninajihisi vibaya.
Mimi pia sikuwa mtu mwema, maana nilikuwa ninafanya kazi saa 10, 12, 14 ili kuepuka yote haya hata siku za wikendi. Kulikuwa na tatizo: Baadhi ya watu hufurahia kunywa pombe -na wengine hufurahia kufanya kazi.
Ni kwanini watu huwa hawaondoki katika mahusiano licha ya kuteswa?
Sababu hizi nne zimeelezwa na mkuu wa kitengo cha kitaifa cha kupokea taarifa za dharura cha Ukraine, Olyna Krivulic, na mshauri wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la idadi ya watu , Olina Kochimirovskaya.
- Watoto wanaolelewa katika familia ambazo zimekuwa na unyanyasaji huwa na mienendo kama ya wazazi wao wanapokuwa watu wazima.
- Hofu ya kubaki peke yao na kuzidiwa na hisia za kifikiria : “Majirani watasema nini?” “Ni wazazi wanapaswa kuwalea watoto pamoja .”
- Hatua ya kwanza – maumivu ya kiakili huwa hayatambuliwi mara moja. Waathiriwa wanajipata wamezoea na kushindwa kuelewa na kushughulikia hali waliyomo.
- Mtu ambaye ni muathiriwa wa unyanyasaji hawezi kwenda kokote kule. Mara nyingi huwa wanamtengemea kipesa mynyanyasaji au wanajipata katika hali ambyo ni vigumu kwao kuondoka kama vile kuwa wajawazito au kuwa na watoto na mnyanyasaji.
Wakati malalamishi yanapotolewa kwa mamlaka, inasikika kwamba “hili ni suala la familia yako ” na hakuna usaidizi utakaoupata.
“Siwezi kuzungumza ‘
Huwa mtu unajipata hufahamu kile kinachotokea wakati unapokuwa katika hali ya aina hiyo. Huoni njia ya kujinasua kwenye mtego na katika hali hii huwezi kumpata mtu wa kukusikiliza. Hufikirii hata kama kuna njia ya kuondokana na tatizo hili.
Niliendelea kufanya kila kitu ambacho sikupenda kukifanya. Nimekuwa kila mara nikimshukuru mtu fulani na sio mimi, Nini wa bibi yangu, mimi ni mtoto wa wazazi wangu-nadhani unapaswa kila wakati kukata tamaa katika mahusiano.
Kwahiyo nililazimika kuacha mambo yangu niliyoyapenda na wakati mwingine lilionekana kuwa jambo la kawaida kwangu. Kwahiyo hali ikaanza kuwa mbaya na mbaya zaidi.
Mwanzoni nilipenda yote haya lakini baada ya miaka mitatu , minne nilianza kuumia kwasababu ya ngono. Ira alikuwa akinivuta kila wakati na nilizazimika kuvumilia maumivu.
Ira alifikiri nina tatizo na ngono. Kwahiyo kila baada ya miaka michache alikuwa ananipeleka kwa daktari wa masuala ya ngono.
Kila mara niliposema sipendi ngono, niliambiwa nina tatizo. Nilikaa kimya dhidi ya janga na nikaendelea kubakwa .
Kwa Ira, kwenda kwa daktari ilikuwa ni kudhihirisha alichokitaka…kuonesha nina tatizo .Mara chache kabla ya talaka hatimaye nilianza kuzungumzia kuhusu unyanyasaji. Nilianza mazungumzo, lakini sikuacha kunyanyaswa.
CHANZO CHA HABARI BBC