Thursday, January 16

Timu ya Wachezaji wa Zamani ya Pemba Veterani Imeibuka Bingwa na Mchezo wa Kirafiki wa Wachezaji wa Zamani Zanzibar kwa Kuwafuna Veterani ya Unguja Kwa Bao 4-2.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Bi. Fatma Hamad Rajab akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Mchezo wa Wachezaji wa Zamani wa Mpira wa Miguu Zanzibar Nahodha wa Timu ya Veterani ya Pemba Suweid Hamad baada ya kuibuma mshindi wa mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Gombani Pemba kwa ushindi wa mabao 4-2 kwa njia ya penenti baada ya timu hizo kutoka sare bila ya kufungana na (kulia) NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Khamis Abdalla Saidi, Bingwa amekabidhiwa Kombe na Shilingi Milioni Mona na Laki Tano.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Bi. Fatma Hamad Rajab akimkabidhi Kombe la Mshindi wa Pili wa Mchezo wa Wachezaji wa Zamani wa Mpira wa Miguu Zanzibar Nahodha wa Timu ya Veterani ya Unguja Nassor Bwanga  baada ya kuibuma mshindi wa Pili wa mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Gombani Pemba kwa ushindi wa mabao 4-2 kwa njia ya penenti baada ya timu hizo kutoka sare bila ya kufungana na (kulia) NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Khamis Abdalla Saidi, Mshindi wa Pili wamepata Kikombe na shilingi Milioni Moja.