Thursday, January 16

Vyakula vya ajabu: Je unaweza kula vyakula hivi?

Kiini tete cha bata ni Chakula hiki maarufu zaidi nchini Ufilipino huitwa Balut

Bila shaka wengi wetu tunafahamu kuwa chakula ni muhimu kwa mwili wa binadamu, hasa inapokuja katika suala la afya nzuri inakubidi ule mlo kamili, ikiwa ni pamoja na vyakula vya kulinda mwili, vya kutia nguvu na joto mwilini na vinavyoujenga, bila kusahau vyakula vyenye madini mbali mbali muhimu kwa miili yetu.

Hata hivyo baadhi ya vyakula hivi vimeonekana kuwa ni vya ajabu kwa baadhi ya watuwasiovila, ama kutokana na muonekano wake , mapishi au hata chanzo chenyewe cha mlo:

Kiini tete chabata

Chakula hiki ni maarufu sana nchini Ufilipino. Iwapo utauhitaji mlo huu basi ukifika Ufilifino usisite kuuliza ni wapi unaweza kupata Balut – kama kinavyofahamika kwa wenyeji.

Kiinitete hiki cha bata huondolewa na kuchemshwa vijusi vya bata vikiwa hai. Na chakula hiki huuzwa sana kwenye migahawa ya chakula kwenye mitaa ya Ufilipino na kwa wanaokipenda wanasema kinaandaliwa na bia.

Wanaopendelea mlo huu wanasema unanoga unapoweka chumvi, pilipili na vinegara. Unatakiwa kunyonya kimiminika kutoka kwa yai na kutafuna kilichomo ndani, ikiw ani pamoja na mabawa, mifupa na kila kitu kilichomo ndani ya kiini tete.

Moyo wa Chatu

Moyo hai wa nyoka aina ya chatu ni chakula maarufu kinachopendwa sana nchini Vietnum.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Moyo hai wa nyoka aina ya chatu ni chakula maarufu kinachopendwa sana nchini Vietnum.

Moyo hai wa nyoka aina ya chatu ni chakula maarufu kinachopendwa sana nchini Vietnum.

Waandaji wa mlo huu, hawana shughuli nyingi, sipokuwa kumchana chatu mbele yako na kuondoa moyo wake ukiwa bado unaendelea na mapigo yake.

Mara nyingi utoaji wa moyo wa chatu hufanyika mbele ya mteja anayetaka kuula wakati ukiendelea kupiga mapigo yake.

Mchanganyiko wa vifaranga mbalimbali vya ndege

ndege

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Chakula hiki huandaliwa kwa kuwauwa mamia ya vifaranga vya na kuwafungwa pamoja ndani ya karatasi ili kuzuia hewa, nzi na funza wasiingie, na baadaye kuuacha mchanganyiko huo kuchacha kwa miezi mitatu.

Harufu ya uvundo wa nyama ya ndege iliyooza inasemekana kuwa na ladha kidogo kama ya jibini iliyokaa muda mrefu.

Chakula hiki huliwa mara kwa mara nyakati za msimu wa majira ya baridi, na katika sherehe maalumu kama vile Christmasi au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.

Chakula hiki kinachofahamika kama Kiviak ni maarufu sana huko Greenland kaskazini wa dunia.

Papa aliyechachishwa

Papa aliyechachishwai ni maarufu zaidi katika jamii ya watu wa Iceland kikiitwa Hákarl

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Papa aliyechachishwai ni maarufu zaidi katika jamii ya watu wa Iceland kikiitwa Hákarl

Chakula hiki ni maarufu zaidi katika jamii ya watu wa Iceland kikiitwa Hákarl. Nyama ya papa ambayo huwa na harufu kali huchachishwa kwa wiki 9 ili kupitia mchakato wa kuchacha ambao humfanya papa kuvunda. Hii humsaidia kupunguza sumu inayopatikana katika nyama ya mnyama huyu, na kuifanya kuwa tayari kuliwa hivyo hivyo bila kupikwa kabisa.

Supu ya nyoka aina ya cobra

Nyoka

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Supu ya nyoka ni chakula ambacho kimekuwa marufu kwa miaka takriban 2,000. Chakula hiki huliwa katika maeneo mbali mbali ya taifa la China , lakini pia katika baadhi ya maeneo mengine ya bara la Asia.

Nyoka wa aina mbali mbali wanaweza kutumiwa kutengeneza supu na mara nyingi wateja hujichagulia ni aina gani ya nyoka wanayotaka watengenezewe supu yake.

Hatahivyo, nyoka maarufu anayependwa ni nyoka aina ya chatu na nyoka wa majini. Nyoka na supu yake huchemshwa kwa muda wa saa sita na chakula hiki kinaaminiwa kuwa cha kiafya na kilichojaa faida za kimatibabu.

Miguu ya vyura

Supu ya miguu ya vyurani chakula kinachopendwa na Wafaransa, pampoja na baadhi ya raia wa Nigeria
Maelezo ya picha,Supu ya miguu ya vyurani chakula kinachopendwa na Wafaransa, pampoja na baadhi ya raia wa Nigeria

Kwa Wanigeria nyama ya chura hupikwa ndani ya supu na kuchanganywa na viazi na wengi hupenda kuongezea pilipili
Maelezo ya picha,Kwa Wanigeria nyama ya chura hupikwa ndani ya supu na kuchanganywa na viazi na wengi hupenda kuongezea pilipili

Huenda ukajiuliza je kweli mtu anaweza kula kitu hiki? Utashangaa kusikia kwamba mamilioni ya vyura huwindwa kutoka maeneo ya misitu na nyikani kila mwaka kwa ajili ya kuliwa na binadamu kila mwaka.

Wafaransa wanaaminiwa kuwa ndio walaji wakuu wa mlo wa vyura unaofahamika zaidi na wenyeji wa Ufaransa kama grenouilles au cuisses de grenouilles. Marekani ni nchi ya pili kwa uuzaji wa wa vyura nje ya nchi , hususan katika maeno ya kusini mwa nchi hiyo ambako vyura wanavunwa zaidi.

Ingawa miguu ya vyura ni chakula cha kawaida miongoni mwa vyakula vinavyopikwa Ufaransa, chakula hiki pia huliwa katika maeneo mengine ya dunia ikiwa ni pamoja na katika maeneo ya Thailand, China, Carribean , Indonesia, na baadhi yamaeneo machache ya Ulaya na Marekani.Chura hukuzwa kwa manufaa ya kibiashara katika baadhi ya nchi kama vile Vietnam. Inasemekana vyura wana kiwango cha juu cha protini, Acid ya mafuta ya , omega-3 yenye wingi wa madini ya Calcium , vitamini A na potassium.

Mende wa kunuka

Wadudu hawa wanaitwa mende wa kunuka kwasababu ya harufu mbaya wanayotoa wakati wanapohisi ishara ya tisho au hatari dhidi yao .

Lakini wadudu hawa ni mojawapo ya vyakula vyenye virutubisho zaidi barani Afrika na wanafikia viwango vyote vya virutubisho vinavyohitajika katika mwili wa binadamu. Wanaokula chakula hiki wanasema ladha kama ya tunda la tofaa(apple)

Baadhi ya wapishi huchanganya mayai ya mende, sehemu nyeupe ya kiini tete cha mende , na watoto wachache wa mende, ili kuongeza ladha ya chakula hiki kinachopendwa sana na wanaokila.

Mboni za macho aina ya samaki tuna

Macho ya samaki aina ya Tuna

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Macho ya samaki aina ya Tuna

Watu wengi humla samaki aina ya tuna, lakini sio kila mtu anayekula mboni za macho. Lakini nchini Japan wanakula macho haya. Wanaokula mboni hizi tuna Huzichemsha ndani ya maji au mvuke. Kisha huzipaka viungo kama vile vitunguu saumu au supu ya soya.

Nyama ya mbwa

Utamaduni wa kula nyama ya mbwa ulianza nchini Uchina miaka 500 iliyopita

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,Utamaduni wa kula nyama ya mbwa ulianza nchini Uchina miaka 500 iliyopita

Katika maeneo mengi hasa ya Afrika na Ulaya , mbwa ni mnyama anayeishi na watu kwa hivyo inakuwa vigumu kumchinja na kumla kama kitoweo. Kwa baadhi wanamuona mbwa wanaomfuga kama sehemu ya familia.

Hata hivyo katika nchi nyingine kama vile Korea Kusini na Kaskazini pamoja na China wenyeji wanakula nyama ya mbwa.

Katika Korea kitoweo hiki maarufu huitwa Boshintang. Nyama hii ya mbwa inaweza kupikwa na supu yenye vitunguu na viungo vingine na inasemakana ni bora kwa afya ya binadamu. Swali ni je unaweza kula kitoweo hiki?.

Mojawapo ya vyakula vya ajabu duniani ni pamoja na supu ya Gaeng kaing Mot Daeng.

Huu ni mchanganyiko wa mayai ya mchwa na viini tete kutoka kwa mchwa weupe na mara nyingine mchwa wachanga kabisa huongezwa ili kuongeza utamu.

Supu hii ni maarufu katika nchi za Uchina, Korea Kusini na Korea Kaskazini.

CHANZO CHA HABARI BBC