NA ABDI SULEIMAN.
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulid Mwita, amesema kuwa kufanyika kwa resi za ngalawa na mbio za baskeli Pemba, ni moja ya ishara ya kutangaza utalii wa kisiwa hicho.
Waziri tabia aliyaeleza hayo wakati alipokua akifungua resi za ngalawa na mbio za baskeli katika kijiji cha Tumbe, ikiwa ni shamrashamra za tamasha la utamaduni wa mzanzibari ambalo hufanyika kila mwaka Kisiwani Pemba.
Akizungumza na wanamichezo hao, alisema kufanyika kwa mashindno hayo ni moja ya ishara muhimu ya kutangaza utalii ya Kisiwa cha Pemba kwa kutumia ngoma mbali mbali za asili.
Alisema kwa hatua hiyo imekuja baada ya kuona michezo hiyo imekua ikipoteza uasilia wake, licha ya waanzishili wake ni kutoka maeneo ya hayo hayo ya Tumbe.
“Sisi huku juu tumeanza kuonyesha njia na ubuf=nifu, tutahakikisha tunaleta na michezo mbali mbali sio hii, kutakua nan age Bich soka”alisema.
Nahodha Kombo Suleiman Zaharan kutoka ngalawa ya Tetema, aliyomba serikali kuhakikisha wanaongeza michezo mengine pamoja na kushajihisha ngalawa nyingi katioka mashindano hayo.
Alisema mashindano ya resi za ngalawa sasa yameanza kupotea kutokana na kutokua na kuwepo kwa boti za kisasa, pamoja na vijana kutokua tayari kurithishwa fani hiyo.
Hata hivyo aliitaka serikali kuandaa mashinano makubwa ya resi za ngalawa yatakayowashirikisha ngalawa kutoka Unguja na Pemba, kama ilivyokua miaka ya nyuma.
Katibu mkuu wizara ya habari utamaduni na michezo Fatama Hamdi Rajab amesema wizara itaendelea kuendeleza mila na utamaduni wa mzanzibar na kuurisisha kizazi hadi kizazi .
Naye adinani Iliyasa Sleimana mshindi wa kwanza katika mbio za baskeli, aliyomba wizara kuhakikisha ijarudisha mashindano ya mbio hizo, pamoja na kuwatafutia wafadhili wa kufadhili kila wakati.
Mshindi wa kwanza katika resi za Ngalawa alikuwa ni ngalawa iana ya Tetema ailiyojinyakulia shilingi laki nne, shindig wa pili ngalawa shinogo ilipata laki tatu, mshindi wa tatu ni ngalawa Zilipendwa iliyopata Pesa laki mbili na washiriki wakipatiwa laki moja moja.
Kwa upande wa seri za baskeli mshindi wa kwanza alikuwa ni Adinani Ilyasa aliyepatiwa zawadio ya silingi Laki 1.5, mshindi wa pili Laki moja tu na msingi wa tatau ni elfu 80000
Tabamasha hilo lilioanzia kwa mbio za baskeli katika eneo la tumbe, yaliyoanzia na mbio za basikali kuanzia tumbe mashariki, konde ,kinyasini lindini hadi kufika katika fukwe za bahariya tumbe ambapo kwa upande wa resi za ngalawa zimekimbizana kwa muda wa saa moja baharini na hatimaye kupatikana washindi