Thursday, January 16

YANGA YAFANYA KUFURU, WAUJAZA UWANJA WA MKAPA, YACHAPWA 2-1 NA ZANACO FC

 

 

NA EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM

Ikiwa leo ndo kilele cha wiki ya mwananchi kwa mashabiki wa klabu ya Yanga ambapo sherehe hiyo imefanyika Jijini Dar  es Salaam wamecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Zanaco Fc ya nchini Zambia ambapo wamefungwa mabao 2-1 licha ya kipindi cha kwanza kuongoza.

Sherehe hiyo ilihudhuliwa na baadhi ya viongozi wakubwa Serikalini akiwmo Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ambaye alipata fursa kuzungumza na mashabiki katika hafla hiyo.

Heritie Makambo alianza kwa kuipatia bao timu yake mnamo dakika ya 30 akipokea pasi kutoka kwa Feisal Salumu ‘Fei Toto” na kuwapeleka Yanga mapumziko wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Yanga ilifanya mabadiliko ya wachezaji kadhaa kwaajili ya kuonesha viwango vyao ndipo wachezaji wa klabu ya Zanaco ikapata mwanya ya kurudisha goli na kuweza kuongeza na lingine na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.