Thursday, January 16

Tetesi za soka Ulaya Jumanne tarehe 31.08.2021: Mbappe, Bellerin, Kounde, Hudson-Odoi, Tagliafico, Edouard

Real Madrid imejiondoa katika mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kutoka Paris St-Germain kwasababu vilabu haviwezi kukubali ada.(RMC Sport – in French)

Hata hivyo, klabu hiyo ya Uhispania inatarajia kuipiku PSG katika mbio za kumsajili kiungo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 18 Eduardo Camavinga kutoka Rennes. (Canal+ via Get French Football News)

Manchester City hawatarajii yeyote zaidi ama kuingia au kuondoka kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa baada ya kumfungia kipa wa Brazil Ederson, 28, kwa mkataba mpya. Kiungo wa Ureno Bernardo Silva, 27, alikuwa ndiye gumzo katika ofa kutoka AC Milan, lakini hakufurahishwa na hatua hiyo. (Times – subscription required)

Hector Bellerin

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Hector Bellerin

Barcelona watajaribu kumsajili beki wa kulia wa Arsenal na Uhispania Hector Bellerin, 26, ikiwa mlinzi wa Brazil Emerson Royal, 22, ataondoka Nou Camp na kujiunga na Tottenham. (Mundo Deportivo – in Spanish)

West Ham wamefikia makubaliano ya maneno na Ajax kumsaini beki wa kushoto Nicolas Tagliafico, ingawa kukamilisha makubaliano hayo kabla ya tarehe ya mwisho uhamisho , Jumanne itakuwa vigumu na mchezaji huyo wa miaka 28 ambaye sasa hivi yuko katika jukumu la kimataifa na Argentina. (Telegraaf – in Dutch)

Hata hivyo, kuna wasiwasi wa Hammers kuendeleza mpango wa kutafuta makubaliano na Tagliafico licha ya beki huyo kutolewa kwa klabu hiyo na mawakala wengi. (Athletic)

Mlinzi wa Sevilla, Mfaransa Jules Kounde, 22, ameibuka kuwa mchezaji wa juu anayelengwa na Manchester United

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Mfaransa Jules Kounde

Chelsea wamemuambia ajenti wa beki wa kati wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde watafanya jaribio la mwisho kumsajili mchezaji huyo wa miaka 22. (ABC Sevilla, via Sport Witness)

winga wa Chelsea na England Callum Hudson-Odoi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Bayern Munich wanamsaka winga wa Chelsea na England Callum Hudson-Odoi

Leicester City wameonyesha nia kwa winga wa Chelsea na England Callum Hudson-Odoi, 20, ambaye pia amehusishwa na Borussia Dortmund. (football.london)

Blues pia wanataka kumchukua kiungo wa Atletico Madrid raia wa Uhispania Saul Niguez, 26, kwa mkopo lakini mabingwa wa La Liga wanataka kujumuisha kifungu ambacho kitaifanya kuwa mkataba wa kudumu kwa £ 34m. (Goal)

Burnley wapo kwenye mazungumzo ya kumleta mlinzi wa Swansea City na Wales Connor Roberts, 25, Turf Moor. (WalesOnline)

Adama Traore

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Adama Traore

Mshambuliaji wa Wolves Adama Traore, 25, amemuajiri wakala Jorge Mendes kumsaidia kupata uhamisho Tottenham. Mchezaji huyo wa Uhispania anataka kuungana tena na kocha wake wa zamani Nuno Espirito Santo. (Footballer Insider)

Wolves wamewasilisha dau la pauni milioni 8.6 kumsajili mlinzi wa Marseille na Croatia Duje Caleta-Car lakini timu hiyo ya Ligue 1 inataka pauni milioni 12.9 kabla ya kumruhusu mchezaji huyo wa miaka 24 aondoke. (Foot01 – in French)

Miralem Pjanic

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Pjanic, (kulia)

Juventus wameamua kutotafuta mkataba kwa kiungo wa kati wa Barcelona na Bosnia-Herzegovina Miralem Pjanic, 31, huku kilabu cha Serie A kikikaribia kumsajili Mholanzi Mohamed Ihattaren mwenye umri wa miaka 19 kutoka PSV Eindhoven. Pjanic, ambaye alikaa Juventus kwa miaka minne kabla ya kujiunga na Barca mnamo mwaka 2020, ni mmoja wa wachezaji kadhaa ambao kilabu hicho cha Kikatalani wanajaribu kumuuza kabla ya tarehe ya mwisho ya Jumanne. (Goal)

Brentford imetoa ofa ya pauni milioni 13 kwa beki wa Gremio, Mbrazil Vanderson, 20, ambaye pia amevutia AC Milan msimu huu. (Goal)

Kiungo wa kati wa Chelsea Tino Anjorin anakaribia kujiunga na Lokomotiv Moscow katika mkataba wa mkopo ambao unajumuisha chaguo la pauni milioni 17 kumnunua Mwingereza mwenye umri wa miaka 19. (Goal)

CHANZO CHA HABARI BBC