“Si mimi pekee niliyetalikiana na mume wangu, bali hata ndugu yangu pia alitalikiana na mwenza wake kwasababu tulikuwa ndugu sote tulioolewa familia moja .”
Haya ni maneno ya Nabibahen Rawal, ambaye alitalikiwa bila sababu kutokana na mila inayotekelezwa katika jimbo la Gujarat inayofahamika kama Satapata.
Walisema kwamba ndoa yao ilikuwa yenye furaha lakini walilazimika kuachana kutokana na mila hii.
Mahakama ilimsaidia kwa hiyo yeye, mume wake na watoto waliweza kuishi tena baada ya kuachana kwa miezi saba.
“Kama mahakama isingesaidia, tungetengena maisha yetu yote yaliyobaki,” Nabibahen aliongeza.
Nabibahen alikuwa ameolewa na shemeji yake Suresh miaka minane iliyopita katika kijiji cha Pora kilichopo katika jimbo la Radhanpur, kulingana na mila ya Satapata.
Kulingana na mila ya jamii ya Rawal ya Gujarat, kaka yake Nabi Jaimal alikuwa amemuoa shemeji yake Suri.
Ndugu wanapoolewa katika familia moja, huitwa , Satapata , awali, ndoa yao ilikuwa vyema.
Mume wake Suribahen Jaimal na mume wake Suresh wote walikuwa wafanyakazi.
“Wifi yangu alimwambia Suribahen kwamba kaka yangu alikuwa mraibu wa pombe. Nilijaribu kumueleza lakini malumbano yalizidi baina yao ,”Nabibahen told BBC Gujarati.
Talaka ya kaka, ilimfanya dada yake kumuacha mume wake
CHANZO CHA PICHA,DINESH KUMAR / EYEEM
Kwa upande mwingine , Suribahen, ambaye aliachana na mume wake, aliiambia BBC Gujarati, “Mume wangu alikuwa akinipiga kila siku kutokana na ulevi. Alikuwa hata haniletei dawa nilipokuwa mgonjwa . nilikuwa nimemchoka.”
“Mume wangu hakuwa tayari kutekeleza majukumu ya kifamilia kwahiyo jamii ikaamua tuachane kwahiyo tuliachana tarehe 15 Januari, 2021.”
“Ndoa yetu ilipangwa kulingana na taratibu za kijamii, kwahiyo kaka yangu pia alinitaliki ,” anasema Suribahen.
“Kwakuwa sheria ni kwamba kama ndoa ya ndugu itafanyika katika familia moja na kama kaka au dada ataachana na mwenza wake, mwingine pia atalazimika kutalikiwa.”
“Baada ya kutalikiana, mume wangu alikataa kuonana na watoto wangu. Kwahiyo nilituma maombi kwa mahakama ya juu ya Gujarat ya malezi ya watoto ,” anasema
Baada ya kushawishiwa, wenzi hao walikubali kusihi pamoja
CHANZO CHA PICHA,MRTHAKKAR
Kaimu Jaji mkuu Vineet Kothari na Jaji Umesh Trivedi katika Mahakama ya juu zaidi ya Gujarat waliwasilisha kesi yao kwa Katibu wa mamlaka ya huduma za kisheria ya wilaya na Jaji mkuu wa Patan MR Thakkar kwa ajili ya kutatua kesi hiyo tata ya mila ya Satapata.
Jaji mkuu wa Patan M.R. alisema “Mchakato wa upatanishi ulikuwa wenye utata kijamii na haikuwa rahisi kupata suluhu ,” Thackeray aliiambia BBC Gujarati.
“Tulipoanza kupatia ushauri nasaha wenza, tulibaini kuwa mzozo wao ulikuwa wa kawaida sana . Mwanaume alikuwa mraibu wa pombe na tukamuelezea kwamba pia hali hii inaharibu maisha ya baadaye ya watoto wake na watoto wa dada yake .”
“Kwasababu wenzi hao waliachana kwasababu ya mila ya Satapata lakini walitaka kuishi pamoja kama mke na mume na hawakuwa na mzozo kati yao .”
“Tuliwaita viongozi wa kijamii na tukawapatia usaidizi wa wakili wa ngazi ya juu Jyotsna Nath ili awashauri madada,” anasema MR Thakkar.
CHANZO CHA PICHA,TOWFIQU BARBHUIYA / EYEEM
Aliongeza kuwa , “Baada ya kazi ngumu, tuliweza kuwashawishi wote (Suribahen na mjume wake) na wakakubali kuoana upya. Baada ya kuoana upya , tuliwasilisha ripoti kwa mMahakama ya ngazi ya juu zaidi na mahakama ikawaruhusu waoane tena upya kulingana na sheria za nchi za ndoa .”
Mila ya Satapata ni nini?
Katika baadhi ya maeneo ya Gujarat, utamaduni wa satapata katika ndoa unadaiwa kuwa umekuwa ukifanyika kwa karne mbili.
CHANZO CHA PICHA,ASHISH KUMAR / GETTY
Mwanahistoria maarufu mwenye makao yake Ahmedabad H.K. ambaye pia ni Mkuu wa zamani wa chuo cha Subhash Brahmbhatt aliiambia BBC Gujarati, “Hasa katika baadhi ya maeneo ya Gujarat Kaskazini , utamaduni huu bado unaendelea hadi leo .”
“Utamaduni huu unapendelewa zaidi miongoni mwa wafugaji .”
“Sababu kuu ni kwamba wakati watu hawa wanaenda kutafuta malisho ya wanyama wao, watoto wao wanaweza kuendelea kutunzwa ,”anasema Subhash Brahmbhatt.
“Kwasababu wale ambao wameoana wanakuwa ni watu kutoka familia moja, ambao ni kaka wa msichana ambaye ameoa dada mmoja lazima amuoe dada yake pia.”
Subhash Brahmbhatt anasema, “Kulingana na utamaduni huu, kama mtu ataachana na mwenza wake ,dada au kaka yake atalazimika kutalikiwa tu, kwahiyo watu hao hilo litawafanya watu hao wasifikirie talaka haraka . Kwahiyo utamaduni huu ulianzishwa kwa lengo la kudumisha sheria ya kijamii.”
CHANZO CHA HABARI BBC