NA ABDI SULEIMAN.
RESI za Ngalawa ni Moja kati ya burudani nzuri na za kuvutia za asili na kiutamaduni, ambazo hufanyika ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba.
Katika miaka ya hivi karibuni burudani hiyo imekua ikipata umaarufu mkubwa, kufuatia juhudi mbali mbali zinazochukuliwa za kuendelea katika kuendelea burudani hiyo.
Katika wilaya ya Micheweni Kijiji cha Tumbe, Resi za Ngalawa zimekua ni maarufu kubwa na kuvutia hisia za wananchi kutokana na umahiri wa waendesha ngalawa hizo.
Nidhahiri kufanyika kwa resi hizo za ngalawa mara kwa mara, tunaweza hata kutangaza utalii wa ndani ya nchini yetu, pamoja na kuwavutia watalii moja kwa moja.
Jumla ya Ngalawa 10 ziliweza kushiriki katika resi hizo, zikiwemo Ngalawa maarufu katika kijiji cha Tumbe, zikiwemo Tetema, ukipenda, Shindege, Alipotupo, Spider, Zilipendwa, Waiyona Iyoo, Kilevu, Mauzo na Jichomeke.
Katika kuhakikisha utalii wa Zanzibar unatangazwa na kuimarika, Wizara ya Habari Viajana Utamaduni na Michezo, imesema itatumia Resi za Ngalawa katika kuutangaza utalii.
Katika kuona adhma hiyo inafanikiwa na kutimia, Waziri ya Habari Tabia Mauli Mwita amesema kufanyika kwa resi za Ngalawa Pemba, ni moja ya ishara ya kutangaza utalii wa Kisiwa hicho.
Kufanyika kwa mashindano haya ni moja ya ishara muhimu ya kutangaza utalii ya Kisiwa cha Pemba, kwa kutumia ngoma mbali mbali za asili.
Anasema kwa hatua hiyo imekuja baada ya kuona michezo huo umekua ikipoteza uasilia wake, licha ya waanzishili wake ni kutoka maeneo ya hayo hayo ya Tumbe.
“Sisi huku juu tumeanza kuonyesha njia na ubunifu, tutahakikisha tunaleta na michezo mbali mbali sio hii, kutakua na nage Bich soka”alisema.
Wizara imeshamiria kuinua sekta ya michezo, ikiwemo michezo ya asili ya vijijini na taifa, ikiwa ni moja ya mipango iliyomo katika sera.
Katika kutilia mkazo mashindano ya Ngalawa ni dhahiri kwamba tutataandaa mashindano na Upande wa Unguja, ili tupate bingwa wa ngalawa kwa Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mohamed Mussa Seif, anasema Wilaya ya Micheweni ni miongoni mwa wilaya zinazoongoza kuwa na manahodha wazuri wa michezo ya Resi za Ngalawa.
“Wilaya hii ndio wilaya ya kwanza naweza kusema katika mchezo huu, serikali kwa sasa inakusudia kwenda kushindana na manahodha wengine ili kupata timu moja ya mchezo huu”alisema.
Wanamichezo kuendelea kuwa walinzi na kudumisha suala zima la amani na utulivu uliopo nchini, utulivu huo unakuwa kivutio bora cha watalii.
Katibu Mkuu wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab, wanakusudia kurudi tena Tumbe kwa ajili ya michezo mbali mbali ikiwemo Nage Beach, resi za ngalawa, kuogolea.
Lengo ni kukuza utamaduni wa mzanzibari kupitia michezo mbali mbali ya Utamaduni, jambo ambalo linawezekana na serikali imetilia mkazo katika suala hilo.
Nahodha Kombo Suleiman Zaharan kutoka ngalawa ya Tetema, ambayo iliibuka mshindi wa kwanza katika mshindano hayo, amesema Ngalawa hiyo imetengenezwa kwa ufundi zaidi na kukimbia kwa kasi kubwa kutokana na wepesi wake.
Michezo ya resi za Ngalawa ni moja ya utamaduni unaovutia wananchi wengin, kutokana na vijana wengi kurisi utamaduni huo kutoka kwa wazazi wao waliokuwa wakicheza.
“Hapa Tumbe mchezo huu umejizoelea mashabiki wengi, kutokana na kuwa unapendwa na unaNgalawa za kushindana na zimetengenezwa maalumu kwa mashindano hayo”alisema.
Ameshauri serikali kuhakikisha wanaongeza michezo mengine, panapotokea mashindano mbali ili kuweza kuibua michezo ikiwemo michezo ya asili ambayo imeanza kufa, ikiwemo karata, bado, zuna na drafti.
Hata hivyo aliitaka serikali kuandaa mashinano makubwa ya resi za ngalawa yatakayowashirikisha ngalawa kutoka Unguja na Pemba, kama ilivyokua miaka ya nyuma.
Mwinyi Rashid Khamis kutoka ngalawa ya Waijua hiyo, maesema kufanyika kwa tamasha la utamaduni na kushirikisha resi za Ngalawa ni nijambo la faraja kwao na kuamsha aria kwa manahodha kufanya mazoezi ya mara kwa mara.
“Mimi ujuzi huu nimeupata kwa baba yangu, wakati alipokua akishiriki katika mashindano akinuchukua, mpaka sasa nimekuwa nahodha mwenyewe na hapa nimeshiriki”alisema.
Tabamasha hilo lilioanzia kwa mbio za baskeli katika eneo la tumbe, yaliyoanzia na mbio za basikali kuanzia tumbe mashariki, konde ,kinyasini lindini hadi kufika katika fukwe za bahariya tumbe ambapo kwa upande wa resi za ngalawa zimekimbizana kwa muda wa saa moja baharini na hatimaye kupatikana washindi