Thursday, January 16

YANGA YASHINDWA KUFURUKUTA DHIDI YA RIVERS UNITED, YACHAPWA 1-0 KWENYE UWANJA WA MKAPA

 

********************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Klabu ya Yanga imeshindwa kufurukuta katika dimba lao la nyumbani baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Rivers United ya nchini Nigeria katika mechi ya awali kufuzu makundi ligi ya mabingwa Afrika.

Mchezo huo ambao Yanga ilionekana kuzidiwa kwa kila idara japokuwa walifanya kosa kosa nyingi katika lango la mpinzani.

Kipindi cha pili dakika za lala salama Yanga ilifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji na kuweza kutawala mchezo kwa dakika 10 za mwisho wa mchezo.