Thursday, February 27

Dr Omar mabingwa elimu Bila malipo.

NA ABDI SULEIMAN.

SKULI ya Dr Omar Ali Juma Sekondari kutoka Wawi, imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Mashindano ya 57 ya Elimu bila Malipo, kwa upande wa Mpira wa miguu baada ya kufikia aalama saba (7) katika mashindano hayo.

Mashindano hayo katika ngazi ya Taifa ilizikutanisha skuli nne, mbili kutoka Pemba na mbili kutoka Unguja ambazo ni Chuwini na Potoa (Unguja), Dr Omar Ali Juma na Gandao (Pemba).

Timu hizo zililazimika kucheza kwa mchezo wa ligi, timu itakayoongoza kwa ponta ndio itakayokuwa bingwa wa mashindano hayo, yaliyokuwa yakichezwa kauwanja wa Michezo Gombani kwa michezo mbali mbali.

Dr Omar ametwaa Ubingwa huo baada ya kuifunga Gando Sekondari mchezo wa Kwanza, akaifunga na Skuli ya Potoa Sekondari na kutoka sare ya bila kufungana na Skuli ya Sekondari Chuowini.

Kwa upande wa Chuwini Sekondari imefanikiwa kushika nafasi ya Pili katika mashindano hayo, nafasi ya tatu ikaenda kwa Timu ya Gando Sekondari na nafasi ya nne ikaangukia kwa Potoa Sekondari.

Nayo skuli ya Msingi Wawi imefanikiwa kutwa ubingwa wa mashindano hayo, nafasi ya pili ikishikiliwa na skuli ya Mchanga mdogo Msingi

Kwa upande wa mashindano ya Urushaji kurusha Mkuki, Wanawake Skuli za Msingi mshindi wa kwanza alikua ni Aisha Ali Omar (Fukuchani), nafasi ya Pili ikaangukia kwa  Mkasi Khamis Juma (Tasini) na mshindi wa tatu ni Sharmila Seif Nassor (Ndijani).

Wanaume kurusha Mkuki mshindi wa kwanza ni Ismail Kassim Ismail (Tumbe), nafasi ya Pili ikaenda kwa Malik Juma Muhamad (Fukuchani) huku nafasi ya tatu ikaangukia kwa Pandu Shaji Pandu (Paje).

Sekondari katika urushaji wa Mkuki mshindi wa kwanza wanwake ni Aisha Salim Kassim (Mbuzini), akifuatiwa na Ridhaa Juma Usugu (Mpapa), nafasi ya tatu ikaenda kwa Ilham Rashid Kombo (Kombeni).

Wanaume sekondari kurusha mkuki nafasi ya kwanza ikaenda kwa Mohamed Haji Kali (Kangani) akifuatiwa na Ibrahim Saleh Juma (Pale) na nafasi ya Tatu ikaangukia kwa Hamid Mohamed Khasmi (Dunga).