Saturday, January 18

Matukio katika picha.

MRATIBU wa Taasisi ya Ifraj Zanzibar Foundation Abdalla Said Abdalla (kulia) akikabidhi banda moja la skuli ya Msingi Maziwa Ng’ombe lenye vyumba viwili vya kusomea wanafunzi, Kaimu Mratibu Idara ya Mipango Sera WEMA Pemba Adam Kombo Nassor, banda hilo lililojengwa na Taasisi ya Ifraji Zanzibar Foundation na kugharimu Milioni 27.(
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, akizungumza na vijana wa Wilaya ya Chake Chake na Mkoani, mara baada ya kumaliza matembezi ya kuadhimisha Mwaka mmoja wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, matembezi hayo yalioanzia Machomanne na kumalizikia viwanja vya Gombani
WASANII wa mziki wa Kizazi Kipya Swaga Kisiwani Pemba, wakiimba wimbo maalumu wa kupongeza Mwaka Mmoja wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, huko aktika viwanja vya Michezo Gombani

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)