NA ABDI SULEIMAN.
VIJANA Kisiwani Pemba wamesema kuwa bado wanaendelea kuwa na imani na uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, kutokana na ahadi zake alizoziweka kwa vijana pamoja na wananchi wa Zanzibar.
Walisema kwa sasa ni mwaka mmoja tu wa uongozi wake, lakini mambo makubwa tayari yameanza kuonekana ikiwemo miradi mikubwa ya maendeleo, ikiwemo Hoteli za Kitalii, barabara za Zanzibar, Viwanda, uwanja wa ndege, Afya, na miradi ya bahari kuu.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumailizika kwa matembezi ya vijana kutoka Machomanne hadi Gombani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Maryam Omar Haji kutoka Wilaya ya Mkoani, alisema vijana bado wanaendelea kuwa na imani na Rais Dk.Mwinyi kutokana na Dhamira yake anayoendelea kuitoa kwa wananchi wa Zanzibar hususan vijana.
Alisema vijana watahakikisha wanaendelea kudumisha amani na utulivu, kwani amani dnio kila kitu katika nchi na kuweza kupiga hatua maendeleo.
Naye Hashili Abdalla Fdhili kutoka Chake Chake, aliwataka vijana wenzake kuwendelea kuwa watulivu, na kumpa muda Rais Dk. Mwinyi kuweza kutekeleza kwa vitendo yale yote aliyoyahidi ili kufikia maendeleo.
Alisema haipendezi kuoa vijana wanavunjika moyo na uongozi wa Dk.Mwinyi, kwani mambo anayokusudia kuyatekeleza ni makubwa na sio ya kufanywa kwa haraka haraka na wakati mmoja.
“Sisi kama vijana tunahitaji tunatakiwa kuwa mstari wambele, kuwa watulivu na wavumilivu katika kuhakikisha maendeleo ya nchi yanapatikana na sio kukurupuka kwa vijana na kusikiliza maneno ya watu wa nnje”alisema.
Akipokea matembezi wa Vijana na kuzungumza nao Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, aliwapongeza vijana hao kwa kuadhimisha mwaka mmoja wa uongozi wa Dkt.Hussein Ali Mwinyi madarakani, kwani ni ishara njema kwao ya kumuunga mkono na kuendelea kuwa na imani nae.
Alisema Dk.Mwinyi ndani ya kipindi cha Uongozi wake wa mwaka mmoja mipango mikubwa imepangwa, ambayo yataweza kufungua barabara ya maendeleo kwa Zanzibar na wananchi wake.
Aidha aliitaja baadhi ya miradi ambayo imekusudiwa kutekelezwa ni pamoja na ukarabati na ujenzi wa madarasa 1131 unguja na Pemba, miradi mikubwa ya maji ambayo yataweza kuondosha tataizo la maji kwa wazanzibari.
Miradi mengine ni pamoja na sekta ya afya ukarabati na ujenzi wa hospitali na vituo vya afya, ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa ili ndege kubwa kuweza kutua Pemba, pamoja na miradi mikubwa itakayoweza kuondosha changamoto za ajira za vijana.
“Miradi hiyo itaweza kuondosha na kuzitatua kwa kiasi kikubwa changamoto za maendeleo ya vijana, vituo maalumu vya kuwaendelea na kuwasaidia vijana ili kufikia maelengo yao”alisema.
Aidha mkuu huyo aliwataka vijana kuendelea kutulia na kuimanini serikali yao, sambamba na kudumisha amani na utulivu nchini, kwani bila ya amani hakuna linaloweza kufanyika.
Akizungumzia suala la chanjo ya UVIKO 19, Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo, ili kuweza kujikinga ma maradhi ya ugonjwa huo unaoendelea kuitesa dunia hivi sasa.
Naye mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, alisema vijana ndio wenye maamuzi ya kufanya nchi iweze kwenda vipi, pamoja na kuendelea kuiyunga mkono serikali katika kuleta maendeleo endelevu ya nchi.
Alisema ili Zanzibar ya Uchumi wa Buluu iweze kufikiwa na Tanzania ya Viwanda, lazima suala la amani na utulivu liwepo bila ya kuwepo hakuna hata kimoja kitakacho weza kufanyika, hivyo vijana munapaswa kuendelea kuenzi amani na utulivu uliopo nchini.
Matembezi hayo yaliweza kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali na Chama, wakiwemo maafisa wadhamini Pemba, huku mada ya dhana ya uzalendo na vijana ikitolewa, pamoja na maendeleo ya uchumi wa bluu na fursa za ajira kwa vijana.
MWISHO