Thursday, January 16

SIMBA YANTANGAZA KOCHA MPYA

 

 

Klabu ya Simba SC imemtambulisha rasmi Pablo Franco Martín raia wa Hispania kuwa kocha wao mkuu akichukua nafasi ya Didier Gomes da Rosa aliyeachana na timu hiyo hivi karibuni.

Franco (41) aliyewahi kuwa kocha msaidizi Real Madrid 2018 amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba SC.

Kabla ya kujiunga Simba SC alikuwa kocha wa Al Qadsia ya Kuwait na amewahi kuwa kocha wa Getafe 2015.