Thursday, January 16

HABARI PICHA: NMB Tawi la Chake Chake yaandaa chakula cha usiku kwa wakuu wa Mikoa, Wilaya maafisa wadhamini na Wakurugenzi ikiwa ni pamoja na kuwaeleza huduma mbali mbali zinazotolewa na Bank hiyo.

MENEJA wa Bank ya NMB Tawi la Chake Chake Hamad Mussa Msafiri (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud (kulia) flana yenye ujumbe wa Uchumi wa Buluu, ikiwa ni mikakati ya Bank hiyo katika kumuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi, wakati wa hafla ya chakula wa Usiku kilichofanyika mjini Chake Chake.
MKUU wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya, akizungumza wakati wa hafla ya Chakula cha Usiku kilichoandaliwa na Benk ya NMB Pemba, kwa ajili ya kuunga mkono Kauli ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kwenye uchumi wa buluu.
AFISA kutoka Benk ya NMB Tanzania Isaac Masusu, akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi Mkuu wa NMB wakati wa hafla ya chakula cha usiku, kilichowashirikisha wakuu wa Mikoa, Wilaya maafisa wadhamini na Wakurugenzi hafla iliyofanyika mjini Chake Chake
AFISA Mdhamini Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Pemba Ibrahim Saleh Juma, akiuliza swali watendaji wa NMB Tawi la Pemba, juu ya mikakati yao katika kusaidia suala la Uchumi wa buluu, halfa iliyoambatana na chakula cha usiku na kufanyika mjini Chake Chake
MKUU wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya, akichukua chakula wakati wa hafla ya kumuunga mkono Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, juu ya uchumi wa buluu hafla iliyoandaliwa na benk ya NMP Tawi la Pemba na kufanyika mjini Chake Chake
MAAFISA wadhamini kutoka Taasisi mbali mbali za serikali Pemba, wakipata chakula cha usiku wakati wa hafla iliyoandaliwa na benk ya NMB Tawi la Pemba, ikiwa ni kumuunga mkono Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)