Thursday, January 16

VIDEO: Wananchi ni lazima kuzingatia suala la kudumisha umoja na mshikamano ulioimarisha mara tuu baada ya uongozi wa awamu ya nane kukaa madarakani – RC Mattar

NA MCHANGA HAROUB-PEMBA.

Mkuu wa mkoa waKusini Pemba Mh,Mattar Zahor Zasoud amesema wananchi ni lazima  kuzingatia sana suala la kudumisha umoja na mshikamano ulioimarisha mara tuu baada ya uongozi wa awamu ya nane kukaa madarakani kwani ndio kitu pekee kitakacho leta maendeleo ya zanzibar.

mh, mattar ameyasema hayo huko katika ukumbi wa baraza la mji chake chake  wakati akifungua kongamano la azaki la kuzungumzia mafanikiao ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wa rais wa ranzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi mh,dk hussein ali mwinyi.

amesema ndani ya mwaka mmoja huu tayari wananchi wameshuhudia juhudi kubwa za rais wa zanzibar katika kuendeleza umoja na mshikamano lakini pia kutekeleza matakwa ya katiba ya zanzibar ya kuwepo serikali ya umoja wakitaifa kitu ambacho kinampa nguvu ya kutekeleza alichokiahidui.

nao washiriki wa kongamano hilo wamemshukuru dk hussein kwa jinsi alivyoanza vizuri na kuonesha kujali makundi yote katika kukuza ustawi wa maisha yao.

kongamano hilo limeandaliwa na mtandao wa jumuiya zisizokuwa za kiserikali pemba na kuwashirikisha jumuiya mbali mbali za kiraiya kisiwani humo.

KUANGALIA VIDEO YA KONGAMANO HILO BOFYA HAPO CHINI.