Thursday, January 16

Demokrasia Makini yaunga mkono hotuba ya Rais Dk. Hussein Mwinyi

Na Takdir Suweid

Chama Cha democrasia makini lakini ofisi ya Zanzibar kimeelezea kujiunga mkono kwa asilimia 100 hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi dkt. Hussein Ali Mwinyi alioitoa hapo juzi katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip uwanja wa Ndege.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari huko ofisini kwake Taveta kuhusiana na mwaka mmoja wa uongozi wa dk.Hussein Ali Mwinyi, Katibu Mkuu wa chama hicho Ameir Hassan Ameir amesema hutuba hiyo imeleta matumaini makubwa kwa wananchi wa Zanzibar.
Amesema miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo katika sekta ya elimu, afya, Maji, umeme na kuwawezesha wajasiriamali wadogo wadogo inatarajiwa kutekelezwa Jambo ambalo litawaondoshea usumbufu wananchi.
Aidha amewaomba wasaidizi wake kumsaidia mh Rais kwa kuwa  waaminifu na waadilifu ili kutimiza azma yake ya kuibadilisha Zanzibar kimaendeleo.
Sambamba na hayo amemuomba Dk Mwinyi kusimamia ili kuhakikisha Fedha zilizotolewa na IMF zinatumika Kama ilivyokusudiwa na watakaobainika kufanya ubadhirifu wachukuliwe hatua za kisheria.
Hata hivyo amewakumbusha viongozi wa vyama vya siasa, dini na asasi za kiraia na wananchi kushirikiana ili malengo ya Serikali yaweze kufikiwa.