Sunday, November 24

COP26: Maneno ya kukwepa na maelewano ya makaa ya mawe, lakini mkataba unaonyesha kuendelea

 

Waandamanaji karibu na mkutano wa wa COP, wakiandamana kuunga mkono waathiriwa wa uchimbaji mafuta

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,Waandamanaji karibu na mkutano wa wa COP, wakiandamana kuunga mkono waathiriwa wa uchimbaji mafuta

Ingawa Mkataba wa Hali ya Hewa wa Glasgow ni jaribio kubwa la kudhibiti ongezeko la joto duniani, mzozo wa dakika za mwisho juu ya makaa bila shaka umegubika mpango huo.

India iliungana na China katika kushinikiza kupunguzwa kwa ahadi hii kuu, ikisisitiza “kupunguza” badala ya “kuondoa”.

Ilikuwa onyesho la ujasiri la msuli wa kisiasa wa kijiografia ambao uliacha nchi zinazoendelea na mataifa ya visiwa na chaguo kidogo ila kwenda sambamba na mabadiliko.

Mkataba huo mpya unakuja siku chache tu baada ya mafanikio mengine mashuhuri ya China.

Jumatano iliyopita shirika la habari la Xinua lilipigia tarumbeta ukweli kwaba nchi hiyo ilizalisha makaa wa mawe zaidi kuliko ilivyofnaya ndani ya siku moja.

Tani milioni 12 zambidhaa hiyo nyeusi zilichimbwa. Inapotumiwa kama kawi, mkaa wa mawe kwa siku hutoa hewa chafuzi ya kaboni inayokadiriwa kuwa sa na ile hutolewa na Irelankwa mwaka mzima.

Huu ndio ukweli wa mambo kuhusu hali ya kaboni inayoathiri ulimwengu kila siku.

Kwa kuzingati hilo, makubaliano yaliyofikiwa hapa baada ya muda kurefushwa majadiliano yalionekana kujikokota katika hali ambayo inatishia maisha ya sayari hii.

Chart

Wapatanishi ambao walifanya kazi usiku kucha kupata mapatano bila shaka hawatakubaliana na tathmini hiyo.

Maandishi halisi ya makubaliano ya mwisho ni ya kimaendeleo, yanazifanya nchi kurejea tena na mipango iliyoimarishwa mwaka ujao

Inafahamika pia kwa kuyataja makaa ya mawe kama chanzo kikuu cha tatizo, kwa mara ya kwanza katika miaka 30 ya diplomasia ya Umoja wa Mataifa.

Pia kuna ongezeko kubwa la fedha kusaidia nchi maskini kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa – na matarajio ya mfuko wa dola trilioni kwa mwaka kutoka 2025, ikilinganishwa na lengo la sasa la dola bilioni 100 za kimarekani kwa mwaka.

Wachunguzi pia wanasema kuna “mwanzo wa mafanikio” kwenye swali kuu la hasara na uharibifu.

Hata hivyo, pia kuna mapungufu makubwa katika mkataba huo.

Kuna vifungu vya weaselly ambavyo vitaruhusu baadhi ya nchi kuepuka kutoa taarifa kuhusu mipango yao ya kupunguza uzalishaji, kulingana na “hali tofauti za kitaifa”.

Kuna wasiwasi kwamba baadhi ya mataifa makubwa yanayoendelea kiuchumi kama India na Uchina yatatumia kifungu hicho kukwepa kutoa taarifa ya mipango yao mwaka ujao.

Wanachama wa ujumbe wa India na China siku ya mwisho -Nyakati za mwisho, chi hizo mbili zikijitahidi kudhoofisha mkataba

CHANZO CHA PICHA,EPA

Maelezo ya picha,Wanachama wa ujumbe wa India na China siku ya mwisho -Nyakati za mwisho, chi hizo mbili zikijitahidi kudhoofisha mkataba

Kwa nchi zilizo mstari wa mbele, bado kuna umakini mkubwa katika kupunguza utoaji wa hewa chafuzi bada ya kuzisaidia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Baadhi ya ahadi za ulimwengu halisi zilizotiwa saini hapa zioonekana kuwa za dhuhaka. Korea Kusini ilitajwa kama nchi ambayo inakaribia kuachana na uzalishaji wa makaa ya mawe katika miaka ya 2030. Lakini serikali ya Seoul kwa unyonge iliashiria kifungu cha ahadi kinachosema “miaka ya 2030 au haraka iwezekanavyo baada ya hapo” kumaanisha kwamba wataacha kuchoma mnamo 2049.