Mtumiaji wa mitandao ya kijamii mwezi uliopita aliona ramani ya shimo jeusi katikati ya bahari ya Pasifiki, jambo ambalo liliibua mijadala, kwa dhana mbalimbali kulinganishwa na shimo hilo.
Hata hivyo , lilitambuliwa katika kisiwa kisichokuwa na watu cha Vostok.
Kisiwa ambacho kipo chini ya Jamuhuri ya Kiribati katikati ya bahari ya Pasifiki.’
Shimo jeusi’ la ajabu lililotokea hivi karibuni katikati ya bahari Pasifiki hatimaye limetoweka.
Nini kilichotokea?
Wakati wa kuangalia ramani ya Google, mtumiaji wa mitandao ya kijamii aligundua kuwa kuna shimo jeusi la ajabu katikati ya bahari ya Pasifiki.
Hata hivyo , shimo hilo jeusi lilionekana kuwa mbali na nchi nyingine za visiwani, jambo ambalo liliwachanganya watu wengi mtandaoni.
Kutokana na hali hilo, dhana nyingi zilifananishwa kuwa sawa na shimo hilo.
Suala hili liliwachanganya watu wengi mitandaoni. Kwa hilo mawazo na mapendekezo yalitolewa ikidhaniwa kuwa hilo laweza kuwa shimo.
Baadhi wakasema kwamba yaweza kuwa ni volkano ya chini ya bahari. Wengine wakafikiria kuwa ni kisiwa cha siri au kambi ya jeshi.
Eneo hilo hatimaye likatambuliwa kuwa kisiwa cha matumbawe kilimita 6440 mashariki mwa Australia, kilicho na msitu mkubwa.
Miti katika kisiwa hiki ni ya kijani kibichi. Na inapoonekana kuwa jeusi kutoka angani, kwa ramani za Google inaonekana kama “shimo jeusi.’
Visiwa vinaongezeka ukubwa katika bahari ya Pasifiki
Wanasayansi kutoka chuo cha Aukland wamegundua kuwa ukubwa wa visiwa kadhaa katika bahari ya Pasifiki unaongezeka licha ya tishio la kupanda maji ya bahari kwa upande mwingine.
Wanasayansi wamegundua kuwa, baadhi ya visiwa vimeongezeka kwa asilimia 8 kwa muda wa miaka 70 iliyopita. Ili kuelewa mabadliko hayo walichunguza picha za setilaiti na taarifa zilizopatikana maeneo hayo.
Watafiti wana matumaini kuwa ushahidi utasaidia visiwa hivyo kukabiliana na ongezeko la joto duniani siku zinazokuja.
Dkt Murray Ford ni mwanajiolojia ya pwani. Anafanya utafiti kuhusu kuundwa na muonekano wa dunia.
“Watu wengine wanaona picha za matumbawe, chini ya matumbawe yale kuna mifupa. Inaweza kuvunjwa na nguvu za mawimbi, au kwa kutafunwa na samaki na mchanga ulio ndani yao unatoka nje. Hii huwa ndio msingi wa kuundwa kwa visiwa,” anaeleza.
Dr. Ford na kikundichake wamekuwa wakizuru baadhi ya visiwa hivyo kwa miaka kadhaa na kunakili mabadiliko ambayo yametokea maeneo hayo.
Picha za setiliti za tangu vita va pili vya dunia zinaonyesha mabadiliko katika kisiwa cha Jeh.
Picha hizi zinaonyesha jinsi ardhi ilibadilika wakati wa kipindi hiki , na jinsi maeneo ambayo yalikuwa ni matumbawe sasa yamegeuka kuwa ardhi.
“Matumbawe yanastahili yawe yenye afya ili visiwa vipate kukua,” anasema Dr Ford.
Ikiwa mfumo wa ikolojia umechoka, hutazaaa matumbawe. Na sio vizuri katika ukuaji wa visiwa au kwa wanyama wanaoyatumia maeneo hayo kama makao.
“Baadhi ya matumbawe yanaweza kukua kwa haraka sana lakini yanaweza kuharibiwa na samaki wapya au mawimbi. Laini kama ni magumu yanaweza kugeka na kuwa mchanga,” alisema.
Usalama matumbawe haya yanatoa kwa viumbe ni muhimu sana.
Itakuwaje siku za usoni?
“Hakuna mtu anaweza kujua muda ambao matumbawe yanaweza kubaki kuwa yenye afya. Kupauka kunaweza kusababisha matumbawe kugeuka na kuwa meupe na kushia baharini. Tindikali baharini nazo zinaongezeka kutokana na kubadilika kwa viwango vya joto baharini,” Dr Ford anaeleza.
“Tunahitaji kupunguza uzalishaji wa gesi ya kaboni na kuzuia kuongezeka kwa joto duniani. Ni kitu kinastahili kufanywa dunia nzima. Ni kitu tunaweza kukifanya sisi sote.”
Licha kwamba kuna ushahidi kuwa baadhi ya visiwa vina uwezo wa kupanuka, hii haimaanishi kuwa hatutaweza kuhoji kuhusu kupanda kwa maji ya bahari. Inakuwa hatari kwa visiwa vya ndani na watu wanaoishi huko.
Lakini kutokana na kuongezeka kwa joto baharini, pwani za visiwa katika bahari ya Pacific vinakumbwa na hatari ya mmomonyoko. Tisho la hilo lipo sehemu matumbawe hayo huishia.
Kufahamu ni visiwa vipi vinapanuka na ni vipi vinapungua itasaidia mataifa ya bahari ya Pacific kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia kundi la wanasayasni wanasema hali sehemu moja ni tofauti na nyingine.
Wataalamu wanasema kuna hitaji kwa kila mmoja kuelewa ni kipi huchangia kukua na kupungua kwa mifumo ikolojia na i kipi tunahitaji kufanya kuilinda siku zijazo.
Hii sio tu kwa maendeleo ya visiwa vinavyopanuka au kinga kutoka kwa matumbawe kuzuia kusombwa kwa pwani. Ni mhimu kuelewa vitu hivi, kuelewa maisha ya majini yanayohifadhi visiwa vya matumbawe.