Saturday, January 4

MKOROSHONI bingwa bonanza la afya la ZAC

WASANII kutoka kikundi cha Mwinyi Mpeku cha Wete wakitoa moja ya igizo lao, katika bonanza la Afya kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani, bonanza lililofanyika Mjini Chake Chake
MCHEZAJI wa Timu ya Chake Chake Star Najati akiruka juu na kufunga goli(kikapu), wakati wa boanza la Afya kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani, bonanza lililofanyika Mjini Chake Chake.
AFISA Mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba Salum Ubwa Nassor, akimkabidhi seti ya Jezi na bahasha ya Fedha Taslimu Kepteni wa Timu ya Mkoroshoni Ali Seif Ali, baada ya kuibuka na mshindi wa kwanza kwa kuichapa Younger Islander bao 2-0.

NA ABDI SULEIMAN.

TIMU ya Mkoroshi United na Chake Chaks Star, imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Bonanza la Afya kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani, baada ya kushindwa Mikwaju ya Penanti 2-0 dhidi ya Younger Islander.

Kwa upande wa Chake Chake Star imeshika nafasi ya kwanza baada ya kuibanjuwa Timu ya Wete Star kwa vikapu 15-7 mchezo uliopigwa Gombani nje.

Mshindi wa kwanza mpira wa Miguu Timu ya Mkoroshoni ilikabidhiwa fedha taslimu, mipira, seti ya jezi na Medali, sambamba na mshindi wa pili.

Kwa upande wa Netball waliweza kupatiwa fedha taslimu, pamoja na vikundi vya mazoezi navyo viliweza kupatiwa zawadi zao katika bonanza hilo.

Kepteni wa timu ya Wete Star Kaije Salim (Dada k) aliwataka waandaji wa mashindano hayo kushirikisha timu nyingi, pamoja na kuwapa muda kwa ajili ya maandalizi ili kufanya vizuri.

Alisikitishwa na Kitendo kinachofanywa na viongozi wa mipira, kwa kutokuzishirikisha timu za Pemba za wanawake katika mashindano mbali mbali ili timu hizo kuonyesha viwango vyao.

Hata hivyo aliwataka wachezaji kulinda afya zao, dhidi ya marazi mbali mbali ikiwemo nyemelizi ambayo yamekua yakiwasumbua wananchi.

Kepteni wa Chake Chake Star Samrat Bakar Yussuf, alisema michezo ni afya, ajira na kuwataka vijana kuelekeza nguvu zao katika michezo na sio kubaki vijiweni.

MWISHO