Wednesday, October 30

CHELSEA YAICHAPA 4-0 JUVENTUS LIGI YA MABINGWA ULAYA

MABINGWA watetezi, Chelsea wameibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Juventus katika mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Stamford Bridge Jijiji London.
Mabao ya The Blues yalifungwa na Trevoh Chalobah dakika ya 25, Reece James dakika ya 55, Callum Hudson-Odoi dakika ya 58 na Timo Werner dakika ya 90 na ushei.
Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 12 na kupanda kileleni ikiizidi wastani wa mabao tu Juventus baada ya wote kucheza mechi tano na zote zinafuzu Hatua ya 16 Bora mbele ya Zenit yenye pointi nne na Malmo pointi moja.