Saturday, January 4

Habari picha, Viongozi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira wajengewa uwezo kwa kupewa mafunzo ya usimamizi wa miradi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akifungua mafunzo ya usimamizi wa miradi kwa Viongozi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa lengo la kuwajengea uwezo kinachofanyika leo Novemba 24, 2021jijini Dodoma ambapo alisisitiza usimamizi mzuri wa miradi hiyo ili kuleta tija.Wengine kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu, Bw. Elisha Msengi na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Bw. Paul Masanja.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga (wa nne kushoto mbele) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya kufungua mafunzo ya usimamizi wa miradi kwa Viongozi hao uwezo yanayofanyika leo Novemba 24, 2021jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi Tanzania (TIPM), Bw. Lwitiko Mwalukasa akitoa mafunzo ya usimamizi wa miradi kwa Viongozi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa lengo la kuwajengea uwezo kinachofanyika leo Novemba 24, 2021 yanayofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga (wa tatu kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi Tanzania (TIPM), Bw. Lwitiko Mwalukasa mara baada ya kufungua mafunzo ya usimamizi wa miradi kwa Viongozi wa Ofisi ya Makamu wa Rais leo Novemba 24, 2021 yanayofanyika jijini Dodoma. Wengine kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Mohammed Khamis Abdulla na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu, Bw. Elisha Msengi (kulia)

(PICHA NA  OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA)