Wednesday, October 30

Mhe. Rais Samia afungua maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani Jijini Arusha na kurejea Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani leo tarehe 23 Novemba 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu matumizi ya Barabara alipotembelea mabanda ya maonesho kwenye maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yaliyofanyika leo tarehe 23 Novemba 2021 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.Wa pili kulia Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza jambo kwa Makamanda wa Jeshi la Polisi alipotembelea mabanda ya maonesho kwenye maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyoanza leo tarehe 23 Novemba 2021 katika Uwanja wa  Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Kushoto no Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene

Viongozi pamoja na Wananchi mbalimbali wa mkoa wa Arusha wakiwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuhudhuria Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyoanza leo 23 Novemba 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu matumizi ya Barabara na Madaraja pamoja na kuvuka katika maeneo hayo  kutoa kwa Watoto wa Shule mbalimbali mkoani  Arusha alipotembelea mabanda ya maonesho kwenye maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika leo tarehe 23 Novemba 2021 katika Uwanja wa  Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. wa pili kulia Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyoanza leo tarehe 23 Novemba 2021 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha Uwanja wa  Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizunguza na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. George Simbachawene kushoto, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.  Khamis Hamza Chillo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro baada ya kufungua  maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika leo tarehe 23 Novemba 2021 katika Uwanja wa  Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi jumla ya Pikipiki 26 kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro kwa ajili ya kuongeza kasi ya kufanya Doria kwa Jeshi hilo, kwenye maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yalioanza leo tarehe 23 Novemba 2021 katika Uwanja wa  Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.  Khamis Hamza Chillo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Dodoma wakati akitokea mkoani Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili  katika Uwanja wa ndege wa Dodoma wakati akitokea mkoani Arusha.