Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said akimkabidhi kitabu cha Historia ya Tanzania, Rais wa Chuo Kikuu cha Potsdam cha Ujerumani Profesa Oliver Gunther, baada ya kumaliza mazunumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Mazizini Jijini Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said amesema Wizara itaendeleza mashirikiano na Wadau mvalimbali wa Elimu ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika Sekta hiyo.
Mhe Simai ameyasema hayo wakati alipokuwa na mkutano na ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Potsdam nchini Ujerumani, katika Ukumbi wa Wizara hiyo Mazizini Mjini Unguja.
Ameushukuru ujumbe huo kwa kuja Zanzibar kujenga mashirikiano ambapo amesema kuna haja ya kujengewa uwezo walimu wao ili nao waweze kutoa elimu bora kwa watoto.
Aidha ameushukuru uongozi wa SUZA kwa kumpatia taarifa juu ya uwepo wa mimea adimu ambayo ipo hatarini kutoweka na kuahidi kufanya ziara katika maeneo hayo pamoja na kukaa na wahusika ili kujadiliana namna ya kuidhibiti isipotee.
Nae Rais wa Chuo Kikuu cha Potsdam cha Ujerumani Profesa Oliver Gunther amesema ni mara yake ya kwanza kuja Zanzibar ambapo amevutiwa kutokana na utulivu na ukarimu wa watu wake.
Aidha amesema Chuo chao kipo tayari kuendelea kushirikiana na SUZA katika nyanja mbalimbali ikiwemo masuala ya computer science pamoja na kuwajengea uwezo walimu ili nao watoe elimu bora.
Amesema Chuo chao kina mahusiano zaidi ya miaka 6 na SUZA ambapo amemuahidi Mhe. Simai kuendeleza mshirikiano hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa masuala ya Utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA, Dr. Abdalla Ali amesema wamegundua kuwepo kwa mimea adimu inayopatikana Zanzibar Pekee katika maeneo ya Kiuyu, Misali, na Shamiani na ipo hatarini kutoweka.
Hivyo ameishuri Wizara ya Elimu kutokana umuhimu wa mimea hiyo kuwa ni tiba, kufanya uwezekano wa kuijifadhi ili iwez kusaidia katika vizazi vijavyo.
Ameshukuru Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa kwa mapokezi mazuri.