Aina mpya ya kirusi cha Corona kilichogunduliwa hivi karibuni ambacho kina orodha ndefu ya mabadiliko ambayo yalielezewa na mwanasayansi mmoja kama ni “ya kutisha”.
Ni mapema na visa vilivyothibitishwa bado vipo zaidi katika jimbo moja nchini Afrika Kusini, lakini kuna viashiria kwamba huenda virusi vya ugonjwa huo vikaenea zaidi.
Nini tunachokifahamu mpaka sasa kuhusu Kirusi hicho?
Kirusi hicho kinaitwa B.1.1.529 na huenda Ijumaa hii Shirika la Afya Duniani (WHO) likakipa kirusi hicho jina la Kigiriki (kama lilivyo kwa kirusi cha Alpha na Delta).
Prof Tulio de Oliveira, mkurugenzi wa Kituo cha Kukabiliana na Magonjwa ya mlipuko nchini Afrika Kusini, alisema kulikuwa na “mfululizo usio wa kawaida wa mabadiliko” na kwamba ilikuwa “tofauti sana” na tofauti aina zingine za virusi ambazo zimeenea.
“Aina hiki cha kirusi kilitushangaza, kina mabadiliko mengi zaidi kuliko ambavyo tulitarajia,” alisema.
Profesa Richard Lessells, kutoka Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini, alisema: “Tunapata wasiwasi kwamba virusi hivi vinaweza kujiimarisha, na kuimarisha uwezo wake kuenea kutoka kwa mtu hadi mtu, lakini pia kinaweza kuepuka mfumo wa kinga.”
Uchunguzi wa kisayansi katika maabara utatoa picha ya wazi, lakini majibu yatakuja haraka zaidi kutoka kwa ufuatiliaji wa virusi katika ulimwengu.
Athari zake zikoje mpaka sasa?
Bado ni mapema kutoa hitimisho la wazi kuhusu athari, lakini tayari kuna ishara ambazo zinaleta wasiwasi.
Kumekuwa na visa 77 vilivyothibitishwa katika jimbo la Gauteng nchini Afrika Kusini, visa vinne nchini Botswana na kimoja Hong Kong (ambavyo vinahusishwa moja kwa moja na watu kusafiri kutoka Afrika Kusini).
Hata hivyo, kuna dalili kwamba kirusi hicho kimeenea zaidi.
Kuna matokeo ya haraka yanaweza kupatikana katika vipimo vya kawaida na ambayo inaweza kutumika kufuatilia kirusi hiki bila kufanya uchambuzi kamili wa maumbile.
Kwa hivyo kwa sasa tumeachwa na virusi vinavyoleta wasiwasi kubwa licha ya uelewa wetu mdogo kuvihusu, na ni moja ambayo inahitaji kuangaliwa kwa karibu na kuuliza maswali ya kina juu ya nini cha kufanya na wakati gani. Somo la janga ni huwezi kusubiri kila wakati mpaka uwe na majibu yote.
Hiyo inaonyesha 90% ya visa katika jimbo la Gauteng vinaweza kuwa tayari vimeshamiri na “inaweza kuwa tayari kuwepo katika maeneo mengine” nchini Afrika Kusini.
Lakini hii haituambii ikiwa kinaenea kwa kasi zaidi kuliko kirusi cha Delta, ni kikali zaidi au kwa kiwango gani inaweza kuepuka kinga ya kinga inayotokana na chanjo.
Pia haituambii ni kwa kiasi gani tofauti kitaenea katika nchi zilizo na viwango vya juu zaidi vya chanjo kuliko asilimia 24 ya Afrika Kusini, ingawa idadi kubwa ya watu nchini humo wamekuwa na maambukizi ya Covid.
Kwa sasa tumebaki na wasiwasi mkubwa kuhusu kirusi hiki, licha ya uelewa mdogo kuvihusu, ni moja ya virusi vinavyopaswa kuangaliwa na kufuatiliwa kwa karibu na kuuliza maswali ya kina juu ya nini cha kufanya na wakati gani. Somo kubwa kuhusu janga la corona ni kwamba huwezi kusubiri mpaka uwe na majibu yote.
CHANZO CHA HABARI BBC