Wednesday, October 30

HABARI PICHA: Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria yatoa elimu kwa jamii katika siku 16 za kupinga masuala ya udhalilishaji wa jinsia.

MKURUGENZI wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria kutoka Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Hanifa Ramadhan Said, akifungua mkutono wa kutoa elimu kwa jamii katika siku 16 za kupinga masuala masuala ya udhalilishaji wa jinsia, kwa wananchi wanaishi katika kisiwa cha Fundo Wilaya ya Wete
WASANII wa Sanaa ya Maigizo kutoka Wete Awena Hamad Khamis (kushoto) na Hudhaifat Ali Amour (kulia), akimpatia kanga mama yake amsomee jina lililoandikwa, akionyesha athari za kutokujua kusoma kwa mtoto wakike, wakati wa utoaji wa elimu kwa jamii katika siku 16 za kupinga masuala masuala ya udhalilishaji wa jinsia, kwa wananchi wanaishi katika kisiwa cha Fundo Wilaya ya Wete.
BAADHI ya wananchi wa Kisiwa cha Fundo Wilaya ya Wete, wakifuatilia kwa makini mkutano wa utoaji wa elimu kwa jamii katika siku 16 za kupinga masuala masuala ya udhalilishaji wa jinsia, kwa wananchi wanaishi katika kisiwa cha Fundo Wilaya ya Wete, mkutano ulioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria zanzibar
AFISA Sheria kutoka Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar Yusra Abdalla Said, akitoa maelezo kwa wananchi wa Kisiwa cha Fundo juu ya Changamoto mbali mbali za udhalilishaji wanazokumbana nazo katika jamii, wakati wa utoaji wa elimu kwa jamii katika siku 16 za kupinga masuala masuala ya udhalilishaji wa jinsia, mkutano ulioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria zanzibar
MMOJA ya Wananchi wa Kisiwa cha Fundo Abdalla Salim Ali, akichangia katika mkutano wa utoaji wa elimu kwa jamii katika siku 16 za kupinga masuala masuala ya udhalilishaji wa jinsia, mkutano ulioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria zanzibar

 

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)