Sunday, November 24

Taasisi na Kampuni zaombwa kutenga fungu maalum kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye ulemavu nchini.

Na, Hassan Msellem, Pemba.

Taasisi na kampuni mbali mbali nchini zimehimizwa kuwasaidia watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kupata haki zao za msingi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Dkt. Omar Dadi Shajak katika hafla ya utoaji wa msaada wa visaidizi kwa watu wenye ulemavu huko Chake Chake Pemba, amesema watu wenye ulemavu wana haki sawa na wale wasio na ulemavu, hivyo basi ameziomba taasisi na kampuni mbali mbali kutenga fungu maalum ili kuweza kuwasaidia watu wenye ulemavu nchini.

        ‘’Nianze kwakuwapongeza sana ndugu zetu TCC kwa msaada wenu huu tunafahamu kuwa kuna makampuni mengi sana yenye uwezo zaidi yenu lakini wanatoa misaada kwenye mambo mengine ikiwemo michezo lakini nyinyi mumeona kuna haja ya kuwasaidia Watanzania wenzenu wenye mahitaji maalum ni jambo la kupongezwa sana na niyasihi makampuni mengine kufata nyao zenu’’ alisema

Kwa upande wake Meneja Mahusiano ya Serikali wa TCC Derick Stanley amesema TCC inathamini mchango wa watu wenye ulemavu katika ujenzi wa taifa, hivyo basi ameahidi kuendelea kutoa misaada mbali mbali kwa watu wenye ulemavu ili kuendelea kuwafariji watu wenye ulemavu nchini.

Nae mjumbe wa washirikisho la watu wenye ulemavu Zanzibar Aziza Alai Mussa ameishuku kampuni ya Sigara Tanzania kwakutoa msaada huo na kwakutambua uwepo wa kundi maalumu ya watu wenye ulemavu nchini sambamba na kuwaomba watu wenye ulemavu kuvitumia ipaswavyo visaidizi hivyo.

        ‘’Tunatoa shukuruani kwa kampuni ya Sigara Tanzania kwakutambua uwepo wa makundi ya watu wenye mahitaji maalum kwani awali makundi haya ambayo aliachwa nyuma kidogo hii inaonesha moyo wenu wa dhati wa kuwajali ndungu zetu wenye ulemavu’’ alieleza

Bright Kiria ni afisa Mahusiano na Mawasiliano TCC amesema kupitia program yao ya ‘’togather Creating Change’’ wameweza kuwafikia watu 2000 wenye ulemavu nchini Tanzania na lengo la kampuni hiyo ni kuendelea kufanya kazi na idara mbali mbali ili kuweza kuwawezesha watu wenye mahitaji maalim nchini.

        ‘’Kupitia program yetu hii ya Togather Creating Change tumeweza kuwafikia watu wenye ulemavu 2000 kwa Tanzania mzima na tunaahidi kushirikiana na idara mbali mbali ili kuwawezesha ndugu zetu kwenye jumuiya hizi’’ aliongeza

Suleiman Mansour ni Mwenyekiti kutoka jumuiya watu wenye ulemavu wa macho Wilaya ya Chake Chake, ametoa wito kwa wanufaika wa msaada huo kuweza kuvitunza visaidizi hivyo ili viweze kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku.

        ‘’Niwahusie wenzangu ambao tumepewa vifaa hivi tusivitumie ovyo tukasema ni kitu cha bure hichi si cha bure vimegharamiwa vifaa hivi vimenunuliwa kwa pesa nyingi kwasababu sisi hatuwezi kuvimiliki’’ alisema kwa msisitizo

Nao baadhi ya wanufaika wa msaada huo wameahidi kuvitumia vyema visaidizi hivyo ili viweze kuwa chachu ya mafanikio katika maisha yao.

Msaada huo umetolewa na kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kupitia kauli mbiu yao ya ‘’Togather Creating Change’’  ambapo umejumuisha vitimwendo 30, fimbo 100 pamoja na magongo 100 ambapo takriban watu wenye ulemavu 2000 nchini Tanzania tayari wamepatiwa visaidizi hivyo.