NA MWANDISHI WETU.
Mkurugenzi wa Chama cha waandishi wa habari Wanawake TAMWA-ZNZ Dkt ,Mzuri Issa amesema mazingira ya kisiasa Nchini Tanzania hivi sasa yanatoa fursa kwa wanawake wengi kuwa viongozi wa Serikali na taasisi binafsi kufuatia Nchi kuongiozwa na Rais Mwanamke ambae ni Mama Samia Suluhu Hassan.
Aliyasema hayo katika ukumbi wa Chama hicho uliopo Tunguu Wilaya ya kati Unguja wakati alipokua akizungumza na viongozi mbali mbali kutoka vyombo vya habari na wawakilishi wa asasi za kiraia.
Kauli hio ya Mkurugenzi huyo imekuja kufuatia uwasilishwaji wa ripoti maalumu iliolenga kuona ni kwa kiasi gani baadhi ya vyombo vya habari vinavyowaandika wanawake katika nafasi za uongozi visiwani Zanzibar.
Alisema kwa mazingira yaliopo hivi sasa ni wazi kuwa Nchi imefunguka na fursa zaidi za wanawake walio wengi kuwa viongozi na wanachopaswa ni kujidhatiti na kuwa tayari kugombea nafasi hizo.
Akifafanua zaidi alisema ushiriki wa wanawake katika nafasi hizo si jambo la kuonekana kuwa kikwazo bali ni matakwa ya dunia yenye dhamira ya kuleta usawa kwa watu wote hivyo hakuna sababu kuona mwanamke anaachwa nyuma.
Sambamba na hayo alitoa wito kwa jamii hususani wana ndoa kuacha dhana potofu yenye lengo la kumkandamiza mwanamke kutokua kiongozi kwa madai ya baadhi wanandoa kudai wanawake wanapokua viongozi hubadilika na kukataa ndoa zao za awali.
Katika hatua nyengine aliwataka viongozi hao wa vyombo vya habari kuhakikisha wanatoa kipao mbele zaidi pamoja na kuwa na sera maalumu kuhakikisha ambayo itawawezesha wanawake wengi kuripotiwa habari zao kila siku.
Awali akiwasilisha ripoti hio ya utafiti mkufunzi wa maswala ya habari Dkt,Abuubakar Rajab alisema utafiti huo mdogo ulijikita kwa magazeti mawili ambayo ni la Mwananchi na shirika la magazeti ya Serikali Zanzibar leo.
Alisema kwa kipindi cha miezi minane kutoka Januari hadi August utafiti huo uliolenga kutazama habari mbali mbali mzilizowagusa viongozi wanawake kwa miezi mine na walitazama magazeti 120 katika ya magazeti hayo habari ambazo zimeandikwa kuhusu viongozi wanawake ni 159 pekee na zote zilizobakia zilikijika kwa upande wa wanaume.
Alisema kwa mazingira hayo bado kuna tatizo kwenye vyombo vya habari la kukutoa fursa zaidi kwa wanawake jambo ambalo linapaswa kuzingatiwa na wasimamizi wa vyombo hivyo hivyo hatima kubadili mtazamo na kutoa fursa zaidi kwa wanawake kwenye vyombo vyao.
Akichangia uswasilishwaji wa ripoti hio Mwenyeki wa wanaume wa mabadiliko Mohamed Jabir alisema a vyombo vya habari vinawajibu mkubwa wa kuwaandika wanawake kwani wao ndio watu ambao wanakabiliana na chanagmoto kubwa katika harakati za kisiasa.
Kwa upande wake mhariri wa Gazeti la Zanzibar leo Ramadhan Makame alisema wameuchukua utafiti huo kama changamoto na kuahidi kuzifanyia kazi katika kipindi kifupi kijacho na anaamini utafiti kama huo ukifanyika tena mwakani basi utakua na matukio mazuri zaidi.