Wednesday, October 30

Matukio katika picha.

MWANASHERIA kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Tawi la Pemba, Siti Habibu Mohamed akizungumza na Mwaandishi wa habari Fatma Hamad Faki (Pemba yaleo) na Zuhura Juma (Zanzibarleo), baada ya kumaliza utoaji wa elimu kwa wanafunzi wa skuli ya Madungu Msingi juu ya siku 16 za kupinga udhalilishaji wa kijinsia.
BAADHI ya wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali vikuu Kisiwani Pemba, wakipitia katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 wakati wa uwasilishaji wa mada juu ya Haki za Binaadamu, Dhana ya Udhalilishaji, kwenye kongamano la siku 16 za kupinga udhalilishgaji kwa wanafunzi hao, lililoandaliwa na kituo cha Huduma za Sheria Pemba.
AFISA Mipangoi kutoka kituo cha huduma za sheria Zanzibar Tawi la Pemba, Safia Saleh Sultani akiwaonyesha wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo Pemba, katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 wakati wa kongamano la siku 16 za kupinga Udhalilishaji kwa wanafunzi hao.
AFISA Mdhamini Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ zanzibari, Thabir Othman Abdalla akifungua kongamano la siku 16 za kupinga udhalilishaji, lililoandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar Tawi la Pemba

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)