Wednesday, October 30

HILI la waamuzi juu ya Rushwa linaangaliwa VIPI?

 

 

NA ABDI SULEIMAN

KATIKA miaka ya hivi karibuni mikakati na juhudi mbali mbali zimekua zikichukuliwa na serikali nawadau wa mpira kwa lengo la kuendelea na kuinua mpira wa miguu zanzibar.

Hali hiyo imekuja kufuatia kuonekana kwa kuanza kushuka hadhi na kukosa hamasa kwa mashabiki wake, huku wengi wakijitokeza na kuunga mkono mashindano ya Ndondo Cup.

Serikali ya awamu ya Nane chini ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ikaweka mikakati madhubuti kuhakikisha michzo Zanzibar inainuliwa, kuanzia ngazi mbali hadi ligi kuu ya Zanzibar jambo lililopeleka kupatikana kwa rais mpya wa shirikisho la mpira Zanzibar (ZFF).

Kama hiyo haitoshi viondozi walilazimika kupadhisha Soksi juu ili kupatikana kwa wadhamini, watakao dhamini ligi kuu ya Zanzibar kwa lengo la kurudisha hadhi yake.

Hayo yote yamewezekana lakini tumekua tukirudi kule kule, kwani vitu vingi vimekua vikijitokeza na kulalamikiwa na wapenzi wa soka au kutokufurahishwa navyo michezoni, ikiwemo waamuzi kuzibeba baadhi ya Timu au kuchezesha chini ya kiwango, matusi uwanjani.

Hayo yote ni madogo kubwa linanolopelekea kuua soka za Zanzibar ni suala zima la Rushwa michezoni, hili miaka yote lilikuwa likifanyika kwa siri kubwa sana naweza kusema hivyo.

Novemba 24/2021 ZFF kupitia barua yake yenye kumbukumbu namba REF.NO.ZFF/T/BAF/NO.VOL/134, kwenda kwa kamisaa Ali Said Ali wa Mchangamdogo, inayosema Kufungiwa kusimamia shughuli za mpira wa Miguu.

Barau hiyo imeendelea kusema, kufuatia kitendo ambacho umekifanya cha kuthubutu kuchukua rushwa kwa viongozi wa KMKM kimepelekea kuitia doa ZFF Pamoja na Waamuzi na kamisaa wenzako kwa ujumla.

“Hivyo basi kwa mujibu wa kanuni za kuendesha Mashindano ya Mpira wa miguu sura ya ishirini na tisa 4, ZFF inakusimamisha kujishughulisha na shughuli zote za kusimamia mpira wa miguu ndani na nje ya Zanzibar kwa muda wote”alisema sehemu ya barua hiyo.

Aidha barua hiyo ilisainiwa na Khamis Hamad Juma Naibu katibu Mkuu, ZFF Zanzibar nakala kutumwa katibu Mkuu wa ZFF Zanzibar, Katibu kamari ya Mashindano na Katibu Bodi ya Ligi.

Kwa mujibu wa sheria ya kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) No:1 ya mwaka 2012, sura ya Tano kifungu namba 36(3)(a), mtu atakuwa amefanya kosa ikiwa mtu huyo amepokea rushwa au kushajihisha au kukubali kupokea au kushajihisha.

Kifungu Namba 36(3)(b) mtu atakua amefanya kosa la rushwa ikiwa ameroa au kukubali kutoa.

JEE!! KAMISAA HUYO ANASEMAJE YEYE

Kamisaa Ali Said Ali ambaye amekumbwa na rungu hilo la ZFF, amekanusha kupokea kwa rushwa kutoka kwa uongozi wa Timu ya KMKM kwa ajili ya mchezo Novemba 22 dhidi ya Yosso Boys.

“Mimi nipotayari kwa lolote ikiwa kuitwa kwenye mamlaka zinazohusika na masuala ya Rushwa nitasema ukweli sijapokea, kama nimepokea aletwe shahidi aliyeshuhudia nikipatiwa hizo fedha”amesema.

Kamisaa huyo alifunguka na kusema hilo lililotokea ni chuki binfsi, ambazo zimekua zikifanywa na mmoja ya wasimamizi wa mpira wa miguu Pemba dhidi yake.

“Mchezo Yosso boys na KMKM ilichezeshwa na Mwamuzi wa kati Ibrahim Ali Ubwa, huku mshika kibendera nambari Moja akiwa Abdalla Said Ali, nambari mbili akiwa Ayubu Mohamed Khatib mimi sikuwa katika mchezo huo hasa, ambao ulimalizika kwa 0-0 muda gani nilipewa pesa”alihoji.

UONGOZI WA KMKM WANASEMAJE WAO JUU YA HILO

Katibu wa Timu ya KMKM Sheha Mohamed Ali, amesema uongozi mpaka sasa haujapata barua yoyote kutoka ZFF, wala hakuna kiongozi wa ZFF wala mwaamuzi ambaye amepatiwa pesa na KMKM ili washinde mchezo.

“Mimi nilifika Pemba Novemba 19 na tulikuwa na mchezo Gombani na Mchezo Mwengine tulicheza Novemba 22, sasa ZFF watuambie mchezo upi tunaoambiwa tulitoa pesa au Rushwa, kama tumetajwa kwenye barua tumetoa rushwa basi watupe na sisi barua yetu tuone adhabu tuliopewa”amesema katibu.

Hata hivyo aliitaka kamati ya Waamuzi na ZFF, kuhakikisha wanakua makini wakati wanapotoa barua zao, kwani zinaweza kuwachafulia jina lao jambo ambalo hawakufanya na kuwatia doa kwa jamii.

ZFF INASEMAJE JUU YA BARUA YA KMKM

Naibu Katibu Mkuu ZFF Zanzibar Khamis Hamad Juma, amesema kuwa yeye alipokea barua kutoka kamati ya waamuzi ya Ali Said Ali, juu ya kufungiwa kwake, wala hakukua na barua ya upande wa Pili KMKM.

“baada ya kufika barua hiyo na kutakiwa kuichapa, nimeichapa kwenye Kompyuta na kuitoa kwa mwamuzi huyo, ila sikupokea barua ya KMKM inayowataka kuadhibiwa kama mhusika wa hilo sakata”alifahamisha.

Aidha amesema kamati ya waamuzi ndio iliyokutana na kuamua kumuadhibu kiongozi huyo, sio ZFF kama ambavyo inaonekana sasa hilo jambo.

KAMATI YA WAAMUZI INAYAPI WAO

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya waamuzi Zanzibar Ali Juma Salum, alisema inamamlka ya kusimamia waamuzi na kamisaa wa michezo na sio timu, walichokifanya wao ni kuondosha sitofahamu baina ya waamuzi wa ndani ya vyumba na Kamisaa anayeshutumiwa.

“Sisi hatuhusiki na kutoa adhabu kwa vilabu, sisi tunahusika na waamuzi na kamisaa, pale tutakapowaona wanaboronga tunawadhibu, kwa kuwafungia au kuwapa onyo”amesema.

Aidha alisema ZFF Pemba kuna matatizo mengi, bodi ya lingi ndio wenyedhamana ya Mpira kusimamia, hata adhabu zote zinazotolewa wao ndio watoaji lakini kazi zao zinahodhiwa na Wengine.

MAMLAKA YA KUZUWIA RUSHWA PEMBA INASEMAJE

Mdhamini wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Pemba Suleiman Ame Juma, alisema ZAECA haijapokea taarifa yoyote ya shutuma au lalamiko lolote la kutokea au kupokea kwa rushwa, kwa kamisaa wa Mpira wa Miguu Pemba kutoka kwa viongozi wa Timu ya KMKM.

“Hapo Mpokeaji na Mtoaji wote walikuwa tayari kupokea na kutoa, kwani hawakufika kutoa taarifa ZAECA juu ya suala hilo, huku akiahidi kufuatilia sakata hilo kiundani ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.

WAAMUZI WANAMTAZAMO GANI WAO

Ali Omar Khamis ambaye jina sio la kwake, amesema alisema suala hilo halikuwa na ukweli wowote, kama lingekua na ukweli na upande wapili ungepatiwa barua, hivyo hizo ni chuki binfasi kwa kamisaa huyo.

Alisikitishwa na kitendo cha kamati ya waamuzi kushindwa kufanya kazi zake kikamilifu, kwani mwamuzi anafika kuchezesha michezo sita bila ya kulipwa chochote zaidi ya kukopwa.

“Kama mtu anachezesha michezo sita ya daraja la kwanza na anakopwa pesa, atashindwa kuchukua fedha kutoka upande mwengine, mipira wengine ndio ajira yao sasa kamati inapaswa kuwasimamia vizuri waamuzi”alisema.

WADAU WA SOKA WANASEMAJE

Juma Khamis Omar kutokana na sakata hilo linaweza kuathiri mwenendo mzima wa ligi, ikiwemo wadhamini kujitoa au kujiweka Pembeni ili kuhofiwa kutiwa aibu.

Alisema katika timu zinazo cheza ligi hiyo, suala la rushwa limekua kubwa kwa baadhi ya timu ili kuweza kushinda, hali inayopelekea kufanya vibaya katika mashindano ya kimataifa kwa kutokua na uwezo.

Ali Omar Haji anasema hali hiyo indio inayopelekea kupoteza hadhi na kuuwa soka la Zanzibar, kwani zipo timu za zinauwezo mkubwa ila zinakandamizwa na timu zenye uwezo kwa kutaka kushinda kwa lazima kufuatia kutumia fedha zao.

MWISHO