Wednesday, October 30

Rais wa Zanzibar Mhe.,Dk.Hussein Ali Mwinyi Ametoa Salamu za Rambirambi kwa Familia ya Marehemu Haji Mkombe Ame.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Mzee Haji Mkombe Ame aliyefariki jana na kuzikwa leo huko kijijini kwao Bambi ya Bondeni, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Katika salamu hizo za rambirambi,  Rais Dk. Mwinyi alieleza kusikitishwa na kifo cha marehemu Mzee Haji Mkombe Ame ambaye alikuwa  Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui Zanzibar na kuiomba familia kuwa na subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba.

Rais Dk. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Haji Mkombe Ame mahala pema peponi,  Amin.

Imetayarishwa na Kitengo cha Habari,

Ikulu Zanzibar