NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.
Wajasiriamali Katika Jimbo la Chambani wametakiwa kufanya upembuzi yakinifu kabla ya kuanzisha miradi ili kuhakikisha miradi hio inaleta tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja wakati alipokuwa akifungua mafunzo kwa wajasiri amali wa Jimbo hilo huko kwa Mtora Jimboni hapo.
Amesema ili kuhakikisha mradi wako unafanikiwa vyema lazima utumie wataalamu ambao wataweza kukuelekeza namna bora ya kuutekeleza ili uweze kukuletea faida.
Kwa upande wao Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Mohammed Abdulrahman Mwinyi na Mwakilishi Mh. Bahati Khamis Kombo wamesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wananchi wa jimbo hilo wanaanzisha vikundi vya ujasiri amali ambavyo vitasaidia kuinua hali zao kiuchumi.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wameushukuru uongozi wa Jimbo hilo kwakuwajali wananchi wake bila ya ubaguzi hivyo wamesema wanaamini kwamba lengo la serikali ya awamu ya nane ya kuinua wananchi wake kiuchumi litaweza kufikiwa.
Mafunzo hayo ya siku tatu ambayo yametayarishwa na Mbunge , Mwakilishi na Diwani wa Jimbo hilo, washiri kiwatapata kujifunza namna ya kutengeneza sabuni, aina mbalimbali za batiki , usindikaji wa pilipili pamoja na matunda mengine.
KUANGALIA VIDEO HII BOFYA HAPO CHINI