NA ABDI SULEIMAN.
WIZARA ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Pemba, imepiga marufuku gari aina ya Noha kujihusisha na kufanya kazi ya kupakia abiria, kupiga debe kama daladala katika maeneo ya Bandarini Mkoani na Wete, jambo ambalo ni kinyume na sheria na kanuni za usajili wa gari hizo.
Alisema zipo gari za Noha zilizosajiliwa kama Tax, Pravate Hir na zipo Noha za watu binafsi ambazo hazikusajiliwa kibishara, lakini zinafanya kazi ya kupakia abiria na kupiga debe kama daladala jambo ambalo ni kinyume na usajili wake.
Akizungumza na Zanzibarleo afisa Mdhamini Wizara hiyo Pemba Ibrahi Saleh Juma, alisema Wizara imelazimika kukutana na wadua wa usafiri na usafirishaji, Jumuiya za Madereva (PESTA) na viongozi wa Wilaya ya Mkoani, kwa le kuepusha kunusuru uvunjifu wa amani ambao ungejitokeza kama gari hizo zingeachiwa.
Alisema Noha zimeruhusia kumpeleka na mkuchukua abiria wake, na sio kupiga debe kama ilivyo sasa, gari yoyote itakayoweza patikana inapakia abiria kama gari za abiria hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kupandishwa juu.
“Shada ni gari za Noha kujitokeza kufanya kazi ambazo hazijasajiliwa, gari za Noha kufanya kazi ya kupakia abiria tena zaidi ya 10 hadi 14, wakati gari hiyo usajili wake ni abiria sita hadi saba”alisema.
Alisema utata umejitokeza katika maeneo ya bandarini gari hizo, kupiga debe kama na kupakia abiria kama gari za abiria, jambo ambalo ni kosa na hazikusajiliwa kwa biashara hiyo, baada ya kufuatilia na kugudua kuwa Noha zianapakia abiria.
“Hazijakatazwa kupakia abiria wao wanaowapeleka au kuchukua ila sio kupiga debe, hakuna gari zinazotoa huduma ya Tax kua na vituo viwili, tumetaka kuwepo na kituo cha Tax Micheweni, Konde, Vituo vya TAX vipo Micheweni, Wete, Konde, Mkoani, pia vituo viwe na viongozi watakao simamia mfumo huo”alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, alikiri kuwepo kwa kilio baina ya madereva wa gari za abiria na gari aina ya Noha kupakia abiria kama daldala na tayari walishakutana na viongozi wa taasisi husika kwa ajili ya suala hilo.
Alisema zipo sheria zinazoongoza Tax, gari za watu binafsi na Private Hire na kuwataka wasimamizi wa gari hizo kuangalia sheria zinavyo sema ili kuepuka adhabu zisizolazima.
“Gari za Tax zina vituo vyao na hakuna gari yenye vituo viwili zaidi ya daladala, sio sahihi NOHA kupakia abiria zaidi ya saba gari itakayokamatwa ni kupandishwa juu kwa sheria zaidi”alisema.
Aliwataka kila mmoja kufuata sheria na kanuni katika kazi yake, na hatoa achiwa mtu kwani ndani yake kunaleta fitna na uvunjifu wa amani kama hatua hazitochukuliwa.
Katibu wa Jumuiya ya wenye magari na madereva pamoja na wafanyakazi wa magari ya Biashara Mkao wa kusini Pemba (PESTA) Hafidhi Mbarka Salim, aliwataka amadereva wa gari za Noha kuhakikisha wanafuata sheria zote za usalama wa barabarani, katika suala la upakiaji wa abiria wanapotoka katika maeneo yao.
Alisema gari hizo zimesajiliwa kupakia abiria kati ya saba na sita, sio kupakia abiria kati ya 14 hadi kumi na tano jambo hilo ni kosa kisheria.
“Hawakatazwi kupakia wageni wao kuwapeleka bandarini Mkoani na kuchukua katika meli abiria wao, wanachopaswa ni kutoa taarifa kama wanawageni wao na sio kupiga debe kama gari za abiria zilivyo”alisema.
Alisema lengo ni kuepusha suala la uvinjifu wa amani katika aneo la bandarini Mkoani, ikiwa ni pamoja na ugomvi unaweza kujitokeza, gari yoyote itaweza kuchukuliwa hatua ikiwemo kufutiwa leseni na kufungiwa kwa gari hiyo.