Sunday, November 24

VIDEO: “kuimarisha utawala bora ni wajibu wa kila mmoja kwa nafasi yake kwa kutekeleza kwa Vitendo misingi ya Utawala bora”RC SALAMA.

 

NA KHADIJA KOMBO –PEMBA                                       

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini  Pemba Mheshimiwa Salama Mbarouk Khatib amesema suala la kuimarisha utawala  bora ni wajibu wa kila mmoja kwa nafasi yake kwa kutekeleza kwa Vitendo misingi ya Utawala bora ili kuimarisha maendeleo ya  Zanzibar.

Akizungumza katika Kongamano  la siku moja lililowashirikisha Wakuu wa Wilaya, MakatibuTawala, Maafisa wadhamini pamoja na Wakuu wa Taasisi mbali mbali Kisiwani Pemba , huko katika Ukumbi wa Hoteli ya Green Foliage Mgogoni Chake Chake ikiwa ni katika shamrashamra za kuelekea siku ya utawala bora amesema tokea mwaka 1964 Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar imekuwa ikiimarisha misingi ya utawala  bora kwani ndio itakayosaidia kuleta maendeleo nchini.

Wakiwasilisha mada juu ya Utawala wa sheria katika kujenga jamii yenye kuwajibika Dk Said Khamis Juma na mada juu ya Uzalendo DR. Godfrey Emiliano Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam wamesema Utawala bora ni dhana ambayo ina mambo mengi ya msingi, ikiwemo uwajibikaji na Uzalendo hivyo hakuna budi kufuata misngi hiyo kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa Ujumla.

Kwa  Upande wao washiriki wa Kongamano hilo wamesema msingi ya utawala bora inahitaji kujengwa kwa vitendo hivyo jamii nayo inahitaji kuelimishwa ili kujenga nguvu za pamoja katika kutekeleza dhana hio ili maendeleo ya haraka yaweze kupatikana.

Jumla ya mada nne ziliwasilishwa katika Kongamano hilo ikiwa ni pamoja na Mgongano wa Kimaslahi  ,Umuhimu wa utawala bora katika kuimarisha uchumi wa Zanzibar, Utawala wa sheria katika jamii yenye kuwajibika, pamoja na uzalendo .

KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI.