NA KHALFAN KHATIB –PEMBA.
Klabu ya waandishi wa habari Pemba (PPC) inakusudua kuendeleza histoaria ya kuwepo kwa amani ya kudumu katika kisiwa cha Pemba kama ilivyokua awali kwa kuilimisha jamii kujua wajibu wao hasa wakati wa harakati za uchaguzi .
Mwenye kiti wa PPC Bakari Mussa Juma amesema hayo katika kongamano la kuhamasisha kudumisha amani ya kweli liliwashirikisha vinngozi wa dini ,vyama vya siasa, na asasi za kiraiya huko katika ukumbi samail gombani Chake chake.
Amesema kisiwa cha Pemba kinasifiwa sana na nchi mbalimbali kwa kudumisha amani ya kweli , hiuvyo ni vyema kurejesha histoaria hio kwa jamii kwenye utamaduni wa kudumisha na kuendeleza amani .
Akiwasilisha mada inayohusu amani Dr Ali Yussuf amesema amani iliopo ni ntunu ya visiwa vya Zanzibar hivyo ni wajibu wa kila mtu katika jamii kuona umuhimu wa amani ili nchi iweze kupiga hatua za kimaendeleo
Kwa upande wa wshiriki wa kongamano hilo wamishukuru PPC kwa kutoa elimu hiyo mapema kwani itaweza kusaidia wanachi kutambua umuhimu wa kudumisha amani wakati wote .
Klabu ya waandishi wa habari Pemba( PPC) imeandaa kongamano hilo la kudumisha amani ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa sauti yangu, amani yangu , hatma yangu.
KUANGALIA VIDEO HII BOFYA HAPO CHINI.