NA KHADIJA KOMBO- PEMBA
Vijana Kisiwani Pemba wametakiwa kuacha tabia ya kujikita katika kusubiri kazi kutoka serikalini badala yake watafute namna ya kuweza kujiajiri katika kazi nyengine mbali mbali za maendeleo zitakazowaletea tija na kuinua hali zao kiuchumi.
Akizungumza katika warsha ya siku moja kwa waafanyakazi wa mahoteli huko Kisiwani Pemba Mkurugenzi Mtendaji Jumuiya ya waajiri Zanzibar ZANEMA Maalim Salahi Salim Salahi amesema Vijana wengi wamekuwa na mawazo kwamba kazi ni zile zinazotolewa Serikalini hivyo hupoteza muda mwingi wa kusubiri kazi hizo jambo ambalo hurudisha nyuma maendeleo yao.
Akizungumzia kuhusu umuhimu wa Masuala ya uhifadhi wa jamii amesema kila mtu unamgusa kutokana na mazingira yake hivyo amewaomba waajiri kuhakikisha wanaliangalia vyema suala hilo kwani linasaidia kwa kiasi kikubwa pale mtu anapomaliza muda wake wa utumishi.
Kwa upande wao washiriki hao wamewaomba Wakuu wa taasisi kuhakikisha wanatimiza haki za waajiri wao huku waajiriwa wakitimiza wajibu wao ili kuondoa migogoro ndani ya kazi ili waweze kufanya kazi kwa amani na kuleta tija ndani ya taasisi.
ANGALIA VIDEO YA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPO CHINI.