Thursday, January 16

Jamii Kisiwani Pemba yaonywa kutokuwadhalilisha watu wenye ulemavu.

Hassan Msellem, Pemba.

Afisa mdhamini ofisi ya makamu wa kwanza wa rais Bwana Ahmed Abuubakar amesema ofisi yake haitomvumilia mtu yeyote atakaemdhalilisha mtu mwenye ulemavu na kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya malezi na makuzi kwa watu wenye ulemavu katika ukumbi wa kiwanda cha makonyo Chake Chake amesema kila mtu ni mlemavu mtarajiwa, hivyo ni vyema kuhakikisha watu wenye ulemavu hawadhalilishwi na badala yake wapewe mashirikiano ili waweze kuishi kwa Amani.

Mapema mwakilishi wa taasisi ya Milele Foundations Ali Rashid Hamad kuna baadhi ya familia hazina uelewa juu ya kuwalea watu wenye jambo ambalo linawapelekea kudumaa kiakili kwakutoendelezwa.

Nae mtaribu wa baraza la taifa la watu wenye ulemavu Mashavu Juma Mbarouk amewaomba wadau walioshiriki katika mafunzo hayo kuwa karibu na watu wenye ulemavu ili kuona wanaondokana na tatizo sugu la udhalilishaji.

Mafunzo hayo ya siku moja yameandaliwa na baraza la taifa la watu wenye ulemavu Zanzibar pamoja na taasisi ya Milele Foundation.