Saturday, January 18

WATALII 69 kutoka Ufaransa wawasili kisiwa cha Pemba na watembelea vivutio vya utalii

 

NA ABDI SULEIMAN.

JUMLA ya watalii 69 wamewasili kisiwani Pemba kwa meli maalumu, kwa lengo la kujionea vivutio mbali mbali vya utalii vilivyomo Kisiwani humo.

Watalii hao raia wa Ufaransa wamewasili Kisiwani Pemba kwa ziara ya siku Moja, kwa kutumia Usafiri wa meli aina ya LE BELLOT, wameweza kutembelea na kujionea vivutio vya utalii.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwapokea watalii hao, kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, alisema ujio wa watalii hao ni kukitangaza kisiwa cha Pemba kiutalii kupitia vivutio mbali mbali vilivyomo.

Alisema ujio wao utaweza kuwanufaisha wafanya biashara na wajasiriamali, kuuza na kutangaza bidhaa na biashara zao kimataifa.

“Kwa sasa ni wazi kuwa Kisiwa cha Pemba kimeanza kufunguka kiutalii, ujio wao utaweza kuonyesha dunia kuwa Pemba kuna vivutio vingi vya Kiutalii, Pemba ni sehemu salama ya watalii kutembea”alisema.

Aidha Mkuu huyo alisema ni meli ya pili hiyo kuwasili katika kisiwa hicho, kwani 2018 meli kama hiyo iliwasilia huku wakiitikia wito wa Rais wa Zanzibar kutaka kuongeza idadi ya watalii kutoka 35,000 hadi laki 150,000 ifikapo 2025.

Hata hivyo aliwataka wajasiriamali Kisiwani Pemba, kujiandaa kuitalii kupitia shuhuli mbali mbali ikiwemo Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.

Afisa Mdhamini Wizara ya Utalii na Mambo ya kale Pemba Zuhura Mgeni Juma, alisema mikakati ya Wizara yake ni kuhakikisha wanavitangaza vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya Kisiwa cha Pemba pamoja na kuibua vivutio vipa.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Tawi la Pemba Abdulla Salim Abdulla, akizungumzia sababu ya meli aina ya LE BELLOT kushindwa kufunga gati katika hiyo, ni kutokana na ukubwa wa meli hiyo kuwa na Mita 130 wakati bandari inamita 11`5.

Alisema kwa sasa serikali ipo katika mpango wa utanuzi wa bandari hiyo, kwa lengo la kuweza kufunga gati meli mbali mbali kubwa na za kimataifa, ikiwemo meli za makontena na kuweza kushusha mizigo ndani ya bandari hiyo.

“Hii ni meli ya kwanza kwa Afrika kwa mwaka huu kuja na watalii, hii inadhihirisha kuwa bandari ya Pemba ni salama kwa meli na abiria wake kuja, hili litaweza kuitanganza Pemba kidunia kuwa sehemu salama kutembea”alisema.

Mdhamini wa kamisheni ya Utalii Pemba Hamadi Amini Ali, alisema kufika kwa wageni hao ni moja ya kutanga dunia kuwa ni sehemu salama kwa wageni, pia kuwa na vuvituo adimu wakiwemo popo wa pemba ambao hawapatikani duniani kokote.

Naye afisa Utumishi wa Wizara hiyo Fatma Salimu Ali, alifahamisha kuw aujio wao kutaweza kuongeza mapato kwa serikali na wafanyabiashara, kwani watalii hao watalipa katika taasisi zinazohusika, kununua biashara kwa wajasiariamali.

Mkurugenzi wa kampuni ya East African Holiday iliyowaleta watalii hapo Pemba Duwe Lazaro Daudi, alisema watalii hao watarudi tena Pemba Disemba 29, kwa kutembelea tena maeneo mbali mbali.

Aidha alishuhuru serikali ya SMT na SMZ katika kusaidia kampuni hiyo inafanikiw akuwaleta wageni hao, ndani ya Visiwa vya Zanzibar na baadae kuelekea Kilwa.

Fatma Khamis Haji mfanyabishara wa Embe katika soko la Matunda Chake Chake, alisema ujio wao utaweza kutanua bishara zao, pamoja na kupata fedha za kigeni.

Naye Mohamed Salehe Ali Muuza haluma maarufu soko la Jua kali Chake Chake, aliipongeza SMT kwa kutangaza Kisiwa cha Pemba kiutalii, pamoja na watalii hao kujuwa ladha ya halua ya Pemba ambayo itakuwa ni kivutio kwa watalii wengine.

Hata hivyo ziara ya watalii hao ndani ya ksiiwa cha Pemba, imezingatia taratibu zote za afya, ikiwemo uvaaji wa barako, unawaji mikono kwa kutumia vitakasa maalumu.

MWISHO