Monday, November 25

JAJI MKAAZI PEMBA AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI AHIDI KUTOA MASHIRIKIANAO DHIDI YAO

NA MARYAM SALUM, PEMBA

WANANCHI Kisiwani Pemba wametakiwa kutoa mashirikiano ya kutosha baada ya kufikiwa na Jaji mkaazi Kisiwani humo, ili kuondokana na kilio walichokuwa nacho  cha muda mrefu jambo ambalo lilisababisha kuzorota kwa kesi mbali mbali zikiwemo  za udhalilishaji.

Hayo yalielezwa na Naibu mrajisi wa mahakama kuu Zanzibar Faraji
Shomari Juma wakati akisema machache kwa waandishi wa habari huko katika ukumbi wa mahakama kuu Chake Chake katika hafla ya kumkaribisha Jaji mkaazi kwa upande wa Pemba.

Alisema ni siku chache  Mahakama kuu Zanzibar kupitia kaimu jaji mkuu ilimteua jaji Ibrahim Mzee kuwa jaji  mkaazi Pemba, ili kunyamazisha kilio cha muda mrefu  kwa wananchi hao na kupelekea kumalizika kwakesi kwa wakati.

Akitoa maelezo ya azma ya ujio wa jaji huyo mkaazi, Naibu mrajisi alisema kwamba zaidi ya miaka mitano nyuma kulikuwa na kilio kikubwa kwa upande wa Pemba kutokana na kukosekana kwa  Jaji mkaazi Pemba ilizifanya kesi nyingi kuzorota.

“Kutokana na kukosekana kwa Jaji mkaazi wa mahakama kuu Pemba
takribani miaka mitano, ili wananchi waondokane na hofu na kilio
walichokuwa nacho muda mrefu, na waone kwamba kilio hicho kinaanza kuondoka,” alisema Mrajisi.

Alisema kwa sasa muda wote Jaji huyo atakuwepo Pemba, kwa shuhuli za kuweza kutatua migogoro na kusikiliza kesi za jinai, rufaa ambazo zilikua zipo.

“Rufaa zimekuwa nyingi sana kutokana na kukosekana kwa Jaji huyo
mkaazi kwa muda mrefu, hivyo kilio chao kitaondoka hivyo tunaomba mashirikiano ili kuwepo kwake   iwe chachu ya kuondoka kabisa vitendo hivyo,” alisema Mrajisi.

Aidha kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha utawala wa mahakama sheria ya mwaka 2018 sheria hiyo inakamati mbali mbali ambazo zimeundwa ili kuboresha mahakama kuwa na maadili mazuri kuanzia ngazi zote kwa watendaji wake, endapo kutakuwa na mtendaji anakwenda kinyume na maadili, mwananchi alete lalamiko lake katika kamati husika kwa Pemba kupitia mrajisi huyo.

Alifahamisha kuwa Serikali imeamua kuweka mahakama na Majaji maalum kwa kesi za udhalilishaji na madawa ya kulevya, ili makusudi kesi za aina hiyo zimalizike ndani ya muda mchache.

Naibu huyo aliwataka waandishi wa habari kutoa mashirikiano kuona kwamba wanaijulisha jamii juu ya ujio wa Jaji huyo, pia wananchi kujua kwamba zipo kamati maalum za maadili za kimahakama kuzitumia ili haki itendeke.

Nae Jaji mkaazi kwa upande wa Pemba Ibrahim Mzee Ibrahim mara baada ya kukaribishwa katika hafla hiyo ya kujitambulisha kwa waandishi wa habari, alisema kuwa lengo  ni kuhakikisha mashauri yote yanayowasilishwa mahakamani hata kwa ngazi ya mahakama kuu
yanasikilizwa kwa haraka.

“Hivyo niiambie tu jamii kwamba kwa vile tayari mahakama kuu Pemba imeshapata Jaji mkaazi tunatoa wito kwa taasisi nyengine zote zile ambazo tunashirikiana nazo katika kufanikisha usikilizaji wa kesi katika mahakama kuu, ziweze kushirikiana nakutimiza kila mtu wajibu wake ili kesi ziende,” alisema Jaji huyo.

Alisema kuwa kuna kesi za jinai ambazo zinaanza mahakama kuu  yale makosa makubwa na zile zinanazotokana na rushwa uhujumu uchumi  ambazo moja kwa moja zinaanzishwa na zinasikilizwa mahakama kuu, ni jukumu la kila mtu kujitayarisha vizuri katika hilo ili kesi hizo ziweze kusikilizwa kwa haraka.

“Kwa mfano wananchi kwa upande wao wasikatae kutoa ushahidi ili kesi zende haraka haraka, Polisi wakamilishe upepelelezi na
uchunguuzi,mashahaidi wataalamu, Ofisi ya DPP wajipange katika
kufanikisha hilo, wataalamu wote tuone kila mtu anatekeleze wajibu wake ili kesi ziweze kwenda kila mtu apate haki yake,”alieleza.

Aliwataka wananchi  wahakikishe kuwa mashauri yote yanayopelekwa
katika mahakama kuu kwa upande wa Pemba  kila mtu anaehusika kwa namnamoja ama nyengine kujitahidi ili kesi hizo ziende kwa haraka kufikia lengo lililokusudiwa.

Hata hivyo Mwandishi wa habari wa ITV  Pemba ,Suleiman Rashid Omar kwa niaba ya waandishi wenzake alimpongeza Jaji huyo kwa kuonesha ukaribu na waandishi wa habari na kumuomba kuwapatia mafunzo mbali mbali ya kisheria ili waweze kuripoti vyema taarifa za kimahakama .

MWISHO.

 


Warning: file_get_contents(): http:// wrapper is disabled in the server configuration by allow_url_fopen=0 in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48

Warning: file_get_contents(http://api.xtrsyz.org/xt-visitor-counter/default.php?domain=www.pembapress.club&time=1732508548): Failed to open stream: no suitable wrapper could be found in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48