Sunday, November 24

MKURUGENZI azitaka taasisi za haki jinai Pemba kumalira haraka kesi za udhalilishaji

NA ABDI SULEIMAN.

MKURUGENZI wa Mashataka Zanzibar Salma Ali Hassan, alizitaka taasisi zianzosimamia haki jinai dhidi ya makosa ya udhalilishaji Pemba, kufanya kazi kwa pamoja ili kuona kesi zianzohusiana na masuala hayo zinamalizika kwa wakati muwafaka.

Alisema haipendezi kuona kesi hizo zinachukuwa muda mrefu kifika mwaka au miaka, bali sasa mikakati yao ni kuhakikisha ndani ya miezi mitatu zinamalizika.

Mkurugenzi huyo aliyaeleza hayo katika kikao kinachuhusisha Taasisi zianzosimamia haki jinai dhidi ya Makosa ya udhalilishaji Pemba, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Madungu mjini Chake Chake.

Mkurugenzi Salma alisema kesi nyingi zilizopo ni umri wa miaka 14 hadi 17 za matukio tafauti yanayotokea kwa jamii, hivyo jamii inapaswa kuwa makini katika kufikisha kesi hizo katika vyombo vya sheria.

Aidha aliwataka wasimamizi hao kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri katika idara zao, ili kuona kesi za udhalilishaji zimapofikishwa zinaweza kumailika mapema.

“Haipendezi kuona taasisi moja inamnyoeshea mwenzake kidole, lazima katika kesi hizi tuwe kitu kimoja katika ufanyaji wetu wa kazi ili kuona jamii inaendelea kujenga imani na taasisi zetu katika kesi hizi”alisema Mkurugenzi.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Mwanamkaa Abdulrahman Mohamed, alisisitiza mashirikiano katika taasisi zote ni muhimu katika kupeleka mbele na ukizipatia sifa taasisi zao.

“Kushirikiana kila mtu kwa ngazi yake kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa, ifi wakati jamii iwe mbele katika kusimamia na kufikisha mashahidi pale wanapohitajika”alisema

Hata hivyo aliwataka watendajoi hao kuhakikisha wanasikiliza kesi hizo, kwa muda mdogo mno na mtu kupatiwa haki yake kwa mujibu wa sheria na kanuni.

Mwendesha mashkata mkuu Mkoa wa Kaskazini Pemba Ramadhani Ali Nassib, Ameishukuru Idara ya katiba na Masaada wa kisheri kuwashirikisha watendaji wa DPP katika utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya masuala mbali mbali ya kisheria.

Aidha aliwataka wananchi wanaofanya suhulu ya kesi za udhalilishaji, kuhakikisha kesi inapofika katika Ofisi ya DPP hakuna sulu bali ni kufuata sheria na kanuni kwa kupelekwa mahakamani.

“Kumekua na wimbi kubwa la wananchi kutaka sulu juu ya kesi zao, sisi tumeamua kutokusikiliza tena masuala hayo bali inapofika kwetu ni kwenda mahakamani tu”alisema.

Naye kaimu afisa Upelelezi Mkoa wa Kaskazini Pemba Mohamed Ali, aliwataka wananchi kuhakikisha wanaziripoti haraka kesi hizo pale zinapotokea katika maeneo yao.

Kwa upande wake Abdalla Yahya Shamhuni kutoka Mahakamani, alisema tayri Mahakama imeshapata hakimu wa mahakama maalumu ya watoto, katika kusimamia kesi za watoto Pemba.

MWISHO