Monday, November 25

Mchakato wa Uchaguzi wa viongozi ACT waanza kwa wagombea kujitokeza kuchukua fomu

Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi ACT wazalendo Muhene Said Rashid akimkabidhi fomu ya kugombe Umakamo Mwenyekiti wa Chama hicho Juma Said Sanan huko katika Afisi Kuu Vuga Zanzibar

Na Talib Ussi

Mchakato wa uchukuaji wa fomu  za wagombea katika chama cha ACT Wazaleno umeanza kwa aliyekuwa mshauri wa chama hicho Juma said Sanani kujitokeza kuchukua fomu ya kugombea nafasi makamo mwenyekiti.

Akizungumza mara bada ya kuchukuwa wa fomu hiyo Mgombea huyo  huko katika ofisi ya chama iliyopo mtaa wa Vuga Mjini Unguja alieleza ameamua kuchukua fomu ya kuomba nafasi hiyo kutokana na kuwa ana uzoefu anazoefu nayo.

“Nia nnayo na Uwezo nnao kwani nimeitumia nafasi hii kwa muda katika chama hichi kabla ya kupisha wengine”, Alisema Juma Sanani.

Alisema anawaomba wapiga kura wamuamini kuwa anaiweza nafasi hiyo na atakuwa akimshauri Mwenyekiti mambo mazuri ya kuimarisha chama.

“Nawaomba wanachama wasiwe na wasiwasi na mimi, endapo nikiipata nafasi hii  nitashirikiana nao katika kutekeleza majukumu ya chama chetu” alisema Mgombea huyo.

Hata hivyo alisema anamiini uchaguzi utafanyika katika hali ya huru na haki ili kuendeleza demokrasia katika chama hicho.

Juma Sanani ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 61 alizaliwa Wete Pemba na kupata Elimu yake ya msingi na Sekondari huko huko, alipata Advince Diploma ya Biashara na kufanyakazi kwa miaka ishirini uwalimu wa Sekondari Visiwani Zanzibar.

Kwa upande wa siasa Sanani aliwahi kushika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar wa chama cha ACT wazalendo, na Baadae kuwa katibu Mkuu Taifa na baada ya kuacha nafasi hizo alipata tena fursa ya kushika nafasi ya Makamu wa Mwenyekiti Zanzibar nafasi ambayo alidumu nayo mpaka wakati wanachama wa CUF waliposhusha Tanga na Kujiunga na ACT na yeye kupewa nafasi Mshauri wa Chama hicho.

Mapema akimkabidhi fomu mgombea huyoo Mjumbe wa kamati ya Uchaguzi Tifa ya chama hicho Muhene Said Rashid alimtaka Mgombea huyo kukamilisha matakwa ya fomu halafu kuirejesha kwenye Ofisi za Tume hiyo zilioko Afisi Kuu Zanzibar si zaidi ya tarehe 17 Mwezi huu ambapo uchaguzi utafanyika January 29 mwaka huu.

Nafasi hiyo Imekuwa wazi kutokana aliyekuwa Makamu Mwenyekiti kujiuzulu Mwazoni wa mwezi wa October Mwaka jana.