Thursday, January 16

Hamad Masoud ajitosa uwenyekiti ACT

Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi Taifa chama cha ACT Wazalendo Muhene Said Rashid akimkabidhi fomu ya kugombea Uwenyekiti wa chama hicho Hamad Masoud Hamad

Na Talib Ussi

Mwanachama mwengine wa ACT wazalendo amechukua fomu ya Kugombea Uwenyekiti wa Taifa chama hicho  huku akiahidi kuongoza chama katika misingi bora katika umoja na mshikamano.

Mwanachama huyo ambaye ni  Hamad Masoud Hamad aliyaeleza hayo mara badaa ya kuomba nafasi hiyo na kukabidhiwa fomu huko katika Ofisi ya chama hicho iliyopo Mtaa wa vuga Mjini Zanzibar

Alisema ameamua kuomba nafasi hiyo kubwa kutokana na muundo mzuri uliopo katika chama hicho ambao umeleta umoja na mshikamano  ambapo alifahamisha  kama yeye akichaguliwa ataendeleza misingi hiyo.

Sambamba na hilo alieleza kuwa endapoatapata nafasi hiyo ataendeleza kiu ya Wazanzibar kuyapata mamlaka kamili ya serikali ya Zanzibar.

“Wazanzibar wanakiu ya kupata Zanzibar yao kuwa dola kamili kwa maana hiyo na mimi nikishapewa jukumu la uwenyekiti tutashirikiana kuongeza kasi ya kudai Zanzibar yetu” alieleza Masoud.

Alieleza kuwa amekuwa akipambana kwa maisha yake kwa siasa  na  kuahidi atahitimisha maisha yake akiwa ndani ya serikali inayoongozwa na chama cha ACT Wazalendo kwani  ndicho kinachowatetea watu na chenye malengo ya kupata mamlaka kamili ya Zanzibar.

Hamad amesema anamini si vibaya kurithi mienendo ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho marehemu malim Seif Sharif Hamad katika kuwatetea wazanzibari ili kufikia malengo ambayo wamekusudia.

“Ni lazma tutunze miradhi siasa za maalim Seif ndizo zitakazoendelezwa  ili iwe sadakatjaria na mimi nikishirikiana na wenzangu  yale malengo ya kisiasa yatatimia.”alisema Hamad.

Hata hivyo alibainisha kuwa ni lazma uwepo msukumo kuhakikisha yale aliyoyawacha maalim yanaendelezwa na kutekelezwa kwa vitendo .

Hamad Masoud Hamad  alizaliwa Ole mnamo Novemba 15 mwaka 1959 na alisoma shule ya msingi ole ana stashahada ya pili ya uhandisi  wa ujenzi .

Hamad alifanya kazi ya ualimu kwa mika 5 na alikwenda masomoni aliporudi alifanya kazi Wizara ya maji kwa mika mitatu       na akihudumu nafasi ya ukurugenzi .

 Katika ulingo wa siasa Hamad alihudumu  katika nafasi mbali mbali za uongozi tokea kuanzishwa kwa vyama vingi mwaka 92 hadi 2014 aliwahi kuwa Waaziri wa Mawasiliano na uchukuazi wa serikali ya Zanzibar mwaka 2010

Wanachama wa wawili wa ACT wazalendo tayari wamejitokeza kuchukuwa fomu ya Uwenyekiti na huku mmoja akichukua nafasi ya umakamu hadi leo, uchukuaji na urejeshaji fomu umeaza tarehe 4 january hadi 17 january.