Friday, January 17

HABARI PICHA: Mwenyekiti wa CCM Mhe. Rais Samia afunga maadhimisho ya kilele cha matembezi ya miaka 58 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar katika uwanja wa Makombeni Mkoani Pemba.

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipokea maandamano ya Vijana wa UVCCM Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar huko katika uwanja wa mpira wa Makombeni Wilaya ya Mkoani.
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipokea maandamano ya Vijana wa UVCCM Zanzibar(hawapo pichani), ikiwa ni shamrashamra za Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, huko katika uwanja wa mpira Makombeni Wilaya ya Mkoani
VIONGOZI wa Mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakifuatilia kwa makini hutuba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa kilele cha matembezi ya Vijana wa UCCM Zanzibar, huko katika uwanja wa Mpira wa Makombeni Wilaya ya Mkoani.
WAZIRI wa Habari Vijana Utaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulid Mwita (mtandio mwenkundu) na waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Lela Mohamed Mussa, wakicheza mziki kutoka kikundi cha BIG Star, wakati wa kilele cha Matembezi ya Vijana wa UVCCM Zanzibar, huko katika uwanja wa Mpira wa Makombeni Wilaya ya Mkoani
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipokea picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, kutoka kwa kiongozi wa matembezi ya UVCCM Abdalla Koti
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassa, akiangalia tunzo maalumu ya heshima aliyokabidhiwa na Katibu Mkuu UVCCM Taifa Kenani Laban Kihomgosi, wakati wa kilele cha Matembezi ya Vijana wa UVCCM Zanzibar, huko katika uwanja wa Mpira wa Makombeni Wilaya ya Mkoani
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassa, akimkabidhi cheti cha heshima Niabu Katibu Mkuu UWT, kwa niaba ya Mlezi wa Matembezi ya Vijana wa UVCCM Zanzibar Mama Mariyam Mwinyi, wakati wa kilele cha Matembezi ya Vijana wa UVCCM Zanzibar, huko katika uwanja wa Mpira wa Makombeni Wilaya ya Mkoani
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassa, akimkabidhi Cheti cha Heshima Habib Rashid kwa niaba ya Vijana wa UVCCM Tanzania bara walioshiriki matembezi Maalumu ya kuadhimisha miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya zanzibar, wakati wa kilele cha Matembezi ya Vijana wa UVCCM Zanzibar, huko katika uwanja wa Mpira wa Makombeni Wilaya ya Mkoani

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassa, akizungumza katika kilele cha Matembezi ya Vijana wa UVCCM Zanzibar, katika kuadhimisha miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, huko katika uwanja wa Mpira wa Makombeni Wilaya ya Mkoani

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)