NA ABOUD MAHMOUD
TIMU za soka ya Simba na Azam FC leo zinashuka dimbani leo kuwania ufalme wa kombe la Mapinduzi mwaka 2022.
Mtanange huo utaanza majira ya saa 2:15 usiku katika uwanja wa Amaan ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ataongoza mashabiki kushuhudia mchezo huo.
Wakizungumzia mchezo huo viongozi wa timu hizo kila mmoja alijinata kushinda na kubeba ubingwa.
Mtendaji mkuu wa timu ya Simba Barbara Gonzalez alisema kikosi chao kipo kamili kupambana na timu yoyote, ili kuhakikisha inachukua ubingwa wa kombe hilo kwa mara ya nne.