Thursday, January 16

Juhudi bingwa Mbunge cup

 

NA ABDI SULEIMAN.

TIMU ya Juhudi imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Mbunge Cup, baada ya kuitandika timu ya Mzingani bao 2-0, mchezo uliopigwa katika uwanja wa Kengeja Skuli..

Mashindano hayo yalioshirikisha timu 20, kutoka katika jimbo la Mtambile na kudhaminiwa na Mbunge huyo, huku Fainali hiyo ikivuta hisia za mashabiki wengi wa soka na kuvuta hisia kubwa kwao.

Akizungumza katika fainali hiyo Mbunge wa Jimbo la Mtambile Seif Salum Seif, alisema lengo la Mashindano hayo ni kuibua vipaji vya vijana, kujenga umoja na mshikamano wa wananchi jimboni.

Alisema lengo jengine ni kupatikana kwa wachezaji bora vijana watakao weza kuiwakilisha vyema jimbo hilo, katika mashindano mbali mbali yatakayokuja.

“Mwisho wa fainali hii ndio mwanzo wa mashindano mengine, mikakati ni kuhakikisha mashindano haya yanakua endelevu, kila kipindi hata zawadi zinaweza kuongezeka”alisema.

Hata hivyo aliwataka vijana kutunza vipaji vyao, kwani mchezo ni ajira kubwa na kujitahidi kutunza afya zao kwa kuepukana na vishawishi mbali mbali.

Katika fainali hiyo mshindi wa kwanza akilabidhiwa kikombe, Shilingi Milioni Moja, mipira 10 na medali, mshindi wa pili alikabidhiwa Laki tano, mipira mitano, seti moja ya jezi, mshindi wa tatu alipatiwa shilingi laki tatu, mipira mitatu, seti ya jezi, mshindi wan ne alikabidhiwa laki mbili, mipira miwili, huku timu ya Mtadoda ikiibuka timu yenye nidhamu na kupatiwa shilingi laki mbili na nuzu na mchezaji bora akipatiwa kiatu.